header

nmb

nmb

Monday, March 4, 2013

DHAHIRA AANZA NA KIBANO CHA LIBOLO ATUPIWA 4-0

Katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Libolo ya Angola, Kipa namba mbili wa Simba Abbel Dhahira, leo ameanza vibaya kibarua chake katika klabu hiyo baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza cha timu yake, huku kipa namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja, akianzia benchi na kutandikwa mabao hayo yote manne. 

Dhaila ambaye alinunuliwa kwa dau kubwa kutoka Uganda akiwa mchezaji wa kulipwa katika klabu hiyo, alikuwa akisumbuliwa na nyonga zaidi tangu alipotua tu katika klabu yake hiyo mpya, akitokea Uganda, mwaka jana.

Aidha kipa huyo amekuwa akisugua benchi katika mechi kadhaa hata za Ligi Kuu ambazo, ambazo baadhi zilionekana kuwa ni rahisi kwake na kuwafanya mashabiki wa soka kubaki na maswali mengi yasiyo na majibu, ''kuwa inakuwaje kipa anunuliwe kwa pesa nyingi na ni wa kimataifa halafu anasugua benchi hata katika mechi rahisi''?.

Haikuweza kufahamika sababu zilizomfanya Kocha wa kikosi hicho kuamua kumwanzisha katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na presha kubwa zaidi na kumuacha kipa namba moja Juma Kaseja, akikaa benchi, hali ya kuwa kipa huyo hajawahi kudaka hata katika mchezo wa ligi kuu tu ya Tanzania Bara, pamoja na kuwa ni kipa bora na ni wa kulipwa.

No comments:

Post a Comment