BREAKING NEWSSSSSSSSSS! CHAMA CHA WAAMUZI CHATIMULIWA
CHAMA cha waamuzi nchini (FRAT) kimeondolewa kwenye jengo walilokuwa wamepanga kutokana na kushindwa kulipa pango
FRAT ambao walikuwa wamepanga kwenye jengo la National Housing Corparation (NHC) lillilopo barabara ya Morogoro Posta wameondolewa leo majira ya saa sita mchana na madalali.
Akizungumza na Lenzi ya Michezo Katibu wa FRAT Charles Ndagala amekiri kutolewa vifaa nje na kusema ni kweli wanadaiwa Shilingi milioni tano ambazo ni kodi ya miezi tisa.
"Ni kweli tunadaiwa na tumetolewa vifaa vya ofisi nje hivyo tunaangalia jinsi ya kuhifadhi vifaa vyetu", alisema Ndagala
Hata hivyo hali ya ukata ndio inaikabili chama hicho kiasi cha kushindwa kulipa kodi kwani hakina vyanzo vya mapato.
Lenzi ya michezo ilishuhudia katibu huyo akipakia vifaa hivyo kwenye gari aina ya canter na kuvipeleka kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF). Tunaendelea kufuatilia kuona nini kimejiri.

Katibu wa FRAT Charles Ndagala (wa pili kulia) akizungumza na mweka hazina wa FRAT (wa kwanza kulia) baada ya kupakia vifaa kwenye gari |
Mmoja wa wanachama Jamhuri Swalehe akisaidia kupakia vifaa kwenye gari |
No comments:
Post a Comment