Gorofa hilo liloanguka jana asubuhi mpaka sasa imeripotiwa watu 18 kufariki Tukio hilo limetokea jana asubuhi baada ya jengo la ghorofa zinazokadiliwa 15 lililokuwa linaendelea kujengwa katika mitaa ya Indira Ghandi na Morogoro kuporomoka na kusababisha taharuki kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo ya katikati ya jiji.
Jengo hilo lililoko katika kitalu Na.166 ni mali ya Raza Ndagji na linajengwa na Kampuni ya Lucky Construction Limited.
jengo hlo limeangukia Msikiti na eneo la Madrasa mitaa ya
Kariakoo wakati watoto wapo ndani yake wanaendelea kujifunza masomo ya Madrasa.
GOROFA HILO LIMEANGUKIA NYUMBA MOJA
AMBAYO IPO JIRANI NA MSIKITI AMBAYO ILIKUWA NA WATOTO WAKISOMA MADRASA,
TAARIFA ZA AWALI ZINASEMA INASADIKIWA HIYO MADRASANA WATU WALIOKUWA
JIRANI AMBAO NI MAMA NTILIE NA WATEJA WAO NI TAKRIBANI WATU SITINI,
MPAKA SASA MAITI 18 ZIMETOLEWA NA
KUPELEKWA MOCHWARI NA MAJERUHI TAKRIBANI 30 WAKIMBIZWA HOSPITALI MBALI
MBALI ZA JIJINI.
Mtoto Maisamali Karim
(6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna
Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira
Gandhi.Picha na Mdau Dande
Francis
Baada ya Tukio Hilo kutokea Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Rais Kikwete alitembelea eneo la tukio
No comments:
Post a Comment