header

nmb

nmb

Monday, February 25, 2013

TANESCO IRINGA ACHENI UZEMBE KAZINI MTAKWISHA JAMANI!!!

  

 Mazoea mabaya  ya mafundi  wa Tanesco mkoa wa Iringa ,hapa wakifanya kazi eneo la posta mjini Iringa  bila kuvaa vitendea kazi

 Fundi wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mjini Iringa  hivi karibuni
Matatizo haya hujitokeza mara kwa mara Je swali la kujiuliza huwa hawawasiliani pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na matengenezo ndio umeme uwashwe? 


jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe wa kizembe kama huu.


Jambo jingine ambalo  waweza  kujiuliza kwanini fundi anafanya kazi  bila kuvaa hata Grops mkononi wala mavazi ya kazi.

No comments:

Post a Comment