Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma
Wimbo la utapeli limevamia kwa kasi ya ajabu katika mkoa wa Iringa baada ya wananchi kutapeliwa kupitia ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma .
Matapeli hao wamekuwa wakiwapigia watu mbali mbali simu kuwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuna pikipiki zimetolewa na Rais Jakaya kikwete kwa ajili ya maofisa ugani na kuwa wao wamebahatika kuzipata mbili hivyo wameamua kuziuza kwa bei ya Tsh milioni 2.5 na kama mteja anahitaji afike ofisi za Manispaa na kwa mkuu wa mkoa kulipa pesa hiyo ili apewe pikipiki na hati yake.
Hata hivyo inadaiwa kuwa baada ya wateja kufika hapo wamekuwa wakiambiwa watoe pesa hiyo nje ya ofisi na wakatafute usafiri wa kubeba pikipiki hizo na ndipo wanapoingizwa mjini kwa matapeli hao kukimbia na kuwaacha wakishangaa .
Matukio hayo yametokea kwa nyakati tofauti katika uzio wa ofisi za Manispaa ya Iringa na ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo watu watatu wametapeliwa akiwemo kijana mmoja wa Kiwere aliyetapeliwa kiasi cha shilingi 200,000 na ushehe za mauzo ya nyanya kwa matapeli hao kujifanya ni maofisi wa polisi ambao wanafanya msako wa fedha za mzungu zilizoibwa jana na kukagua fedha za kila mwananchi na hivyo kutaka fedha za mkulima huyo kuchunguzwa huku yeye akisubiri nje ya ofisi za Manispaa ya Iringa kabla ya matapeli hao kutokea mlango wa pili na kukimbia
No comments:
Post a Comment