Askari wa usalama barabara nao washangaa kuona ajali kama hii katikati ya mji
Mmiliki wa gari aina ya RAV 4 iliyogonga gari na kulipanda juu akiwa haamini kilichotokea
Huyu ndie mmiliki wa RAV4 inasadikika ni mfanyakazi wa Tanroads mkoa wa Iringa
Dereva wa Taxi yenye namba za usajili T 510 AYUKelvin Kaduma akiwa salama kabisa
Wazungu ambao ndio wanatengeneza magari nao wakifika kushangaa ajali hiyo ya maajabu
Dereva aliyegongwa na gari aina ya RAV 4 yenye namba T 319 AFLBw Kalvin kaduma ambaye alikuwa akiendesha Taxi yenye namba T 510 AYU amejitokeza kuelezea chanzo cha ajali hiyo na jinsi ambavyo alivyonusurika kifo.
Kaduma anasema kuwa alishuhudia gari hilo RAV 4 hiyo ikija kwa mwendo wa kasi na ndipo alipoamua kusimama ili kushuhudia na ghafla alijikuta akifunikwa na RAV 4 hiyo.
Alisema kuwa RAV 4 hiyo iliruka ukingo la barabara ambao una michongoma na kujengwa kwa sementi na kutua juu ya Taxi yake na kushindwa kuendelea na safari na kuwa iwapo asingesimama kuona mtiti wa gari hilo basi dereva huyo wa RAV4 angekufa kwa kugonga nyumba iliyopo jirani ambayo ina hoteli ya Hast Tast .
Hata hivyo amesema hana mchumbuko wowote na kuwa dereva huyo wa RAV 4 kwa sasa anashikiliwa na polisi baada ya kushindwa kukimbia kutokana na pombe. Kwa hisani Francis Godwin Blog
No comments:
Post a Comment