header

nmb

nmb

Monday, December 3, 2012

MASHINDANO YA MAKASIA YA BALIMI

December 3, 2012
 washiriki wa mashindano ya mitumbwi ya Balimi Extra Lager kutoka katika mikoa ya Mara,Kagera,Kigoma,Ukerewe na Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja kupata maelekezo juu ya namna ya ushiriki wa mashindano hayo kwenye Ziwa victoria
 washiriki wa mashindano ya mitumbwi ya Balimi Extra Lager kutoka katika mikoa ya Mara,Kagera,Kigoma,Ukerewe na Mwanza wakiwa kwenye mstari wa kuanza mashindano hapa wakisubri filimbi ya kuanza kwamashindano hayo ambapo mkoa wa kagera uliibuka washindi.
 Mabingwa wa kanda ya Ziwa wa mashindano ya Mitumbwi ya balimi timu ya mkoa wa kagera wakiwa katika mstari wa kumaliza mashindano hayo na kuwa mabingwa wapya wa balimi kanda ya Ziwa na kufanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi milioni mbili na laki saba
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili na laki saba nahodha wa timu ya Kabanga Group ya kagera Bwana Eliud Prosper Sambamba na zawadi ya kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa wa kanda ya ziwa kwenye mashindano ya balimi boat race .
 mabingwa wa mashindano ya balimi boat race 2012 timu ya mkoa wa mara wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo na viongozi mbalimbali wa TBL Kutoka kushoto ni meneja wa bia ya Balimi Edith Bebwa,Meneja masoko wa TBL Fimbo Butalla kulia malaki sitaki
mabingwa wa mashindano ya balimi boat race 2012 timu ya mkoa wa kagera wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo na viongozi mbalimbali wa TBL Kutoka kushoto ni meneja wa bia ya Balimi Edith Bebwa,Meneja masoko wa TBL Fimbo Butalla kulia malaki sitaki.

TIMU ya Kionga Nyamisi ya Musoma, Mara kwa upande wa wanawake na ile ya Kabanga Group ya Bukoba, Kagera kwa wanaume juzi zilifanikiwa kushinda katika Mashindano ya Kupiga Makasia ya Balimi yaliyofanyika jijini hapa.
 
Mashindano hayo yaliyofanyika katika Ziwa Victoria kwenye eneo la Mwaloni, yalishuhudia umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia timu mbalimbali kutoka mikoa ipatayo mitano zikichuana kuwania ushindi.
 
Kutokana na ushindi huo timu ya Kabanga Group walizawadiwa Sh milioni 2.7, huku Kionga Nyamisi wao wakitoka na Sh milioni 2.
 
Timu zilizoshiriki mashindano hayo zilitoka katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Mara pamoja na Ukerewe ambao ulipewa hadhi ya mkoa katika michuano hiyo.
 
Nafasi ya pili na ya tatu kwa upande wa wanawake ilishikwa na timu za Kakelenga Group (Ukerewe) na Riagamsilwe (Mara), wakati kwa upande wa wanaume zilikuwa Cheka na Weusi (Mwanza) na Lwakazi Group (Kagera).
 
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evaristi Ndikilo aliyekuwa mgeni rasmi, aliwapongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kudhamini mashindano

No comments:

Post a Comment