TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
Desemba 21, 2012
KUZINDULIWA KWA KINYWAJI CHA ZANZI CREAM LIQUEUR
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited wazalishaji wa bidhaa bora zaidi za vinywaji vikali na mvinyo hapa nchini, kwa mara nyingine tena inapenda kutambulisha bidhaa yake mpya ambayo ni kinywaji chenye radha nzuri kabisa kiitwacho Zanzi Cream Liqueur.
Kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kinazalishwa na Tanzania Distilleries Limited, hivyo kuwa kinywaji cha kwanza katika vinywaji vya jamii ya Cream Liqueur kuzalishwa nchini Tanzania na kampuni ya humu nchini na kuingia katika soko la kimataifa kama vilivyo vinywaji vingine vya aina hiyo vinavyozalishwa kutoka nje.
Zanzi Cream Liqueur ni kinywaji cha watu wa aina zote ingawa uzoefu unaonekana aina hiyo ya vinywaji vinapendwa zaidi na wanawake, kutokana na radha yake, humfanya mnywaji ajisikie mwenye furaha muda wote na mambo mengi ya kuvutia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema, ana uhakika kinywaji hicho kitapendwa na wengi kwani ni cha Kitanzania, na kuwa TDL imezingatia ubora wa kiwango cha Kimataifa katika kuzalisha kinywaji cha Zanzi Cream liqueur.
Mgwassa aliwataka Watanzania kujivunia kinywaji hicho, ambacho kimezinduliwa leo na kusema TDL ikiwa ni kampuni ya kizalendo itaendelea kuhakikisha inazidi kuitangaza Tanzania kwa kuzalisha bidhaa bora zinazopendwa na wengi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu sisi TDL tunajivunia kuzindua rasmi kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kwani kinazalishwa na Watanzania na kimebuniwa na wazalendo wa nchi hii, huu sasa ni wakati wa kutembea mbele kujivunia kinywaji hiki na naamini kitavutia wengi kutokana na jinsi kilivyotengenezwa na ubora usio na shaka.”
Mgwassa alisema, nia ya kuzalisha kinywaji cha Zanzi Cream Liquer ni baada ya kuona kuna vinywaji vingi vya aina hiyo vikiingizwa nchini kutoka nje hivyo, TDL ikataka kuzalisha bidhaa bora zaidi na ya kipekee hapa duniani.
Naye Meneja Masoko Taifa wa TDL, Joseph Chibehe alisema kinywaji hicho kitapatikana katika chupa zenye ujazo wa 750ml na Pakiti zenye ujazo wa 100ml, huku kikiuzwa kwa bei ambayo watu wengi wataimudu.
Chibehe alisisitiza kwamba kinywaji hicho kitapatikana kote nchini na watahakikisha kinapenya katika soko la Kimataifa, ili kuitangaza Tanzania juu ya vinywaji bora zaidi vi
KIM, RENARD KUWAKABILI WAANDISHI KESHO
KIM, RENARD KUWAKABILI WAANDISHI KESHO
Makocha wa Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen na Zambia (Chipolopolo) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 21 mwaka huu) kuzungumzia pambano lao litakalochezwa Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makocha hao watazungumzia maandalizi yao ya mwisho kabla ya pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia makocha hao watajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu pambano hilo litakalokutanisha timu hizo ambazo zimefanya vizuri kwenye orodha ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) vilivyotolewa jana (Desemba 19 mwaka huu).
Wakati Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika wamepanda juu kwa viwango vya ubora kwa nafasi nne, Taifa Stars ambayo katika mchezo uliopita iliifunga Kenya (Harambee Stars) bao 1-0 imepanda kwa nafasi nne.
Taifa Stars ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini tangu Desemba 12 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo kubwa ya kirafiki inayotarajiwa kuwa ya kuvutia.
TENGA ATOA NOTISI YA MKUTANO MKUU TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.
NUSU FAINALI UHAI CUP KUPIGWA KARUME
Mechi za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa kesho (Desemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai itazikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Azam na itafanyika kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Simba na Coastal Union zitacheza nusu fainali ya pili kuanzia saa 10 kamili jioni kwenye uwanja huo huo. Mtibwa Sugar imepata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-1 wakati Simba iliilaza Oljoro JKT mabao 2-0.
Nayo Azam iliindoa JKT Ruvu kwenye robo fainali kwa bao 1-0 huku Coastal Union ikipata ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya robo fainali.
Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Mechi ya mshindi wa tatu itaanza saa 2 kamili asubuhi wakati ya fainali itakuwa saa 10 kamili jioni.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA TWFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Desemba 19 mwaka huu) hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Ushindi aliopata Lina Kessy aliyechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TWFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TWFA, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za chama hicho kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Mama Ombeni Zavala na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia Katiba ya TWFA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma (Katibu), Zena Chande (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF) wakati mjumbe wa Kamati ya Utendaji ni Triphonia Temba.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpi
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MMILIKI NA VIONGOZI WA KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA LEO IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia bada ya mkutano wa na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais
NHC YATANGAZA TAREHE YA KUANZA KUUZA NYUMBA ZA BEI POA KIBADA,KIGAMBONI DAR
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe akitangaza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, muda wa kuanza kuuza nyumba 290 za bei nafuu zinazojengwa Kibada, Kigamboni zitakazoanza kuuzwa Januari 2, mwakani. Kulia ni Meneja Masoko na Utafiti wa NHC, Itandula Gambalagi. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo uliofanyika leo NHC Kanda ya Kinondoni
David Shambwe ( wa Pili kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Muungano Saguya ambaye ni Corporate Social Responsinbility Manager, Meneja wa Mkoa wa NHC Kanda ya Kinondoni, Erasto Chilambo na Meneja Masoko na Utafiti wa NHC, Itandula Ga
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo uliofanyika leo NHC Kanda ya Kinondoni
David Shambwe ( wa Pili kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Muungano Saguya ambaye ni Corporate Social Responsinbility Manager, Meneja wa Mkoa wa NHC Kanda ya Kinondoni, Erasto Chilambo na Meneja Masoko na Utafiti wa NHC, Itandula Ga
RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA KABOYONGA
Baadhi ya waombolezaji wakielekea makaburini wakati wa mazishi ya mbunge wa zamani wa Tabora mjini, marehemu Siraju Juma Kaboyonga katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Siraju Juma Kaboyonga.
Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Mare
MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA HUDUMA YA BIMA YA AFYA KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya kwa vikundi vya SACCOS vya UVIMA (Umoja wa vikundi vya WAMA Tawi la Majohe lililoko wilayani Ilala) na Salma Kikwete SACCOS kilichoko Mkuranga. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina (katikati) na kulia ni Afisa wa WAMA ndugu Tabu Likoko akifuatiwa na Grace Michael, Afisa Habari wa Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiangalia moja ya kadi ya mwanachama wa bima ya Afya mara tu baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima hiyo kwa wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012. Wengine katika picha kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Husein Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina na Mkurugenzi wa Mfuko huo Ndugu Emmanuel Humba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa Bibi Tatu Ngao, Mwenyekiti wa UVIMA mara tu baada ya kuzindua rasmi mpango huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.
Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi akimpatia tuzo ya Shujaa wa mfuko wa Bima ya Afya kwa mwaka 2012 Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA kwa jitihada zake kubwa za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kijamii na pia katika kupigania afya kwa wote na hasa makundi maalum ka
KUMEKUCHA MISS EAST AFRICA KUNYAKUA DOLA 30,000 MLIMANI CITY KESHO
Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Event Limited Bw Rena Calist akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Seaescape iliyoko Mbezi Afrikana jijini Dar es salaam wakati akizungumzia matayarisho ya mwisho kabla ya shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika kesho Desema 21 kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Katika shindano hilo wanashiriki warembo kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na na baadhi ya nchi jirani na ukanda h ambapo mshindi wa shindano hilo anatarajiwa kujinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za Kimarekani elfu thelathini 30,000.
Kushoto ni Guetano Kagwa ambaye atakuwa MC wa shindano hilo na kulia ni Serge Nkurunzinza Mwakilishi wa Miss East Africa nchini Burundi .
Guetano Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kulia ni Rena Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo.
JESHI LA POLISI LATOA SIKU SABA KWA BAADHI YA ASKARI POLISI WANAODAIWA KUIBA MILIONI 150 ZILIZOPORWA
JESHI la Polisi limetoa siku saba kwa baadhi ya askari kuzisalimisha fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es Salaam juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili kujua ukweli wa madai hayo.
Alisema Jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kamanda Kova alisema jeshi hilo lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.
Alisema tukio hilo halikubaliki hivyo kila aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka shaka kwa wanachi.
Kova alimtahadharisha Msangi kuwa, endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue hata yeye itabidi awajibike ambapo alisema vitu kama hivi vikiachwa viendelee vinaliletea jeshi hilo sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.
“Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo Msangi lakini hata mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli”alisema Kova.
Alibainisha kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo, ni vema wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.
Aidha, Kova alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi zake kwa nidhamu, uaminifu na ueledi kwani endapo ofisa au askari atakiuka maadili ya kazi yake, basi hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yake bila kuchelewa.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa, eti lifanya kazi kwa kutii sheria zote bila kwenda kinyume.
No comments:
Post a Comment