header

nmb

nmb

Thursday, November 29, 2012

fastjet yazinduliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na kukamilisha makubaliano ya Ubia na Swissport


Shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu Afrika, fastjet, limeizundua ndege yake ya kwanza ikiwa nachapa yake kamili, siku mbili tu kabla ya kuanza safari za anga Tanzania. Kwenye hafla iliyofanyikakwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kamabarage (JKIA),Dar es Salaam, maafisa wa serikali, watendaji wa fastjet na wataalamu wa safari za anga walishuhudia ndege aina ya Airbus A319 ikipaa kwenye anga ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Kuanzia Alhamisi, 29 Novemba, fastjet itafanya safari mbili kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo – Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza, zote zikiwa ni safari zenye wasafiri wengi wa ndani. Tiketi zilianza kuuzwa wiki mbili zilizopita na fastjet imeshuhudia mahitaji makubwa, zaidi kuliko matarajio ya awali. Mpaka sasa idadi ya tiketi zilizonunuliwa ni sawa na safari 60 za ndege iliyojaa, na mauzo yanaendelea kwa safari za mwakani. Nauli zitakuwa za wastani wa dollar $80, lakini zinaanzia bei ya chni kabisa ya $20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali kwa wateja watakowahi kununua tiketi.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winter, alisema:

“Leo ni siku ya kusisimua sana, na siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika, shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama na ubora.”

Akizungumzia uzinduzi huo, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Airbus – Wateja, alisema:

Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”

Fastjet itakuwa ikiendeshwa na timu yenye uzoefu wa safari za ikiongozwa na Ed Winter, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa zamani wa kampuni ya easyjet na mkurugenzi mwanzilishi wa shirika la ndege ya bei nafuu la Go, Afisa Biashara Mkuu Richard Bodin, Mkurugenzi wa zamani wa Mikataba wa easyJet na Mkurugenzi wa Biashara wa shirika la ndege la bei nafuu la Jet2.com, Mkurugenzi wa Uendeshaji Rob Bishton, Rubani Kiongozi & Mkuu wa Shughuli za Ndege wa easyJet na Meneja Mkuu wa Afrika Kyle Haywood, amabye aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Air Uganda.

Shirika hili la ndege linaendeshwa chini ya leseni ya chapa ya easyGroup Holdings Limited na Sir Stelios Haji-Ioannou, mwanzilishi wa shirika la ndege kinara kwa nauli nafuu, easyJet.

Akizungumzia uzinduzi, Mwenyekiti wa easyGroup Holdings, Sir Stelios alisema:

Sasa ni zamu ya Afrika! Nimefurahi kuwa nimeshiriki, japo kidogo, kwenye kuanzishwa kwa mapinduzi mengine tena. Ninawatakia wahusika wote safari njema!”

Shirika hili la ndege linabashiri kwamba idadi ya abiria wa Fly540, ambayo kwa sasa ni abiria 750,000 kwa mwaka, itaongezeka mara dufu ndani ya miezi sita kuanzia uzinduzi huu. Fastjet imepanga ndani ya mwaka mmoja itakuwa na idadi ya ndege 15 aina ya A319.

Kituo cha kwanza cha fastjet niDar es Salaam, na cha pili kitakua niNairobi,ambacho kinatarajiwa kuzinduliwamwakani. Baada ya kujizatiti Afrika Mashariki, shirika hilo la ndege linatarajia kuzinduliwa Accra, Ghana na Luanda, Angola.

astjet pia inafurahi kutangaza kwamba leo imetiliana saini mkataba na Swissport International, shirikia linaloongoza kwenye huduma za sekta ya anga viwanjani, ambapo itakuwa ikihudumia mtandao wote wa shirika hilo la ndege kwa mahitaji yake kwenye viwanja vya ndege.

Kupitia makubaliano hayo ya kipekee ya ubia, Swissport ambayo hutoa huduma mbalimbali kwenye viwanja vya ndege, itawajibika kwa usambazaji na usaidizi wa mlolongo wa ugavi kwenye mtandao wote wa fastjet.

Juan Jose Alvez, Makamu wa Rais Mtendaji wa Uhudumiaji kwenye Viwanja vya Ndege Ulaya, Mashariki ya Kati, Asia na Afrika alidokeza:

“Swissport ina uzoefu mkubwa wa kutoa huduma kwenye mfumo wa usafiri wa bei nafuu katika bara laUlaya na tuko tayari kushirikianakuisaidia kuijenga chapa ya fastjet katika bara laAfrika, kwa kutumia  uelewa na michakato yetu. Ubia huu unahusisha changamoto zote zinazohusiana na uanzishwaji wa mtandao wa kushughulikia ndege kwenye viwanja vya ndege na mifumo ya usimamizi, na hivyo ubia huu ni wa kipekee na unawakilisha aina mpya ya uhusiano kati ya mtoa huduma na shirika la ndege na kutoa firsa kwaSwissport kuendelea kujenga mtandao wake Afrika kwa ubia na fastjet.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Ed Winter alidokeza:

“Swissport ina hadhi inayong’ara kimataifa na historia ya kutoa huduma bora kwa mashirika ya ndege kwenye viwanja vya ndege kote duniani. fastjet inajenga shirika la ndege la bara la Afrika likiwa na viwango vya kimataifa vya usalama, ubora, ulinzi na kuaminika na hivyo ni muhimu kwetu kuwa na mbia ambaye atoakipaumbele cha juu kwa viwango vya ubora kulingana na malengo yetu ya kababmbe ya kustawi barani Afrika.”

No comments:

Post a Comment