Usafiri wa Treni ya abiria leo umeanza rasmi jijini Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi huku kukiripotiwa kuwepo na vituko vya hapa na pale hassa kwenye upande wa upandaji wananchi wakionekana kugombea kama wanavyofanya kwenye daladala. Vituko vyengine ni kuonekana kwa watu wengi kwenye vituo vya treni hiyo pamoja na kuwepo kwa daladala ambazo hazijajaa lakini watu waliendelea kusubiri usafiri wa treni. Kwa mujibu wa Afisa habari wa Shirika Relli (TRL) Midraji Mahezi amesema treni imeanza kusafirisha abiria leo mapema kwa kiwango cha nauli ya Tsh400 kwanza huku taratibu za kutofautisha nauli kulingana na umbali zikiendelea. Huduma hii itakuwepo kuanzia majira ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 5:00 mchana na kuanzia saa9:00 jioni hadi usiku. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea. |
No comments:
Post a Comment