header

nmb

nmb

Monday, October 29, 2012

KISIWA CHA MUSILA KILICHOKUWA GEREZA HIKI HAPA.

Raha za pwani kama kawaida pamoja na kukuletea habari mbalimbali za kitaifa biashara burudani na michezo lakini pia haiachi kukuletea rojorojo za Pwani. Leo hii tunakuletea rojorojo za pwani ya Ziwa Victoria eneo la Bukoba almaarufu kwa jina la Spice beach.


Kisiwa cha Musila ambacho ni upande unaonekana tu, huku upande wapili ukiwa hauna kitu na ukionekana mwamba tu, kama ukijaribu kupanda juu kabisa ya kisiwa lazima utadondokea kwenye maji upande wa pili kwa umbali mrefu. Sehemu yenye mabanda ndiyo sehemu pekee ambayo watu huishi.
Kwa wale waliowahi kufika kwenye fukwe hizo watakubaliana na mimi kwamba ukiangalia upande wa matokea jua utaona kijikisiwa kidogo hivi! basi rojorojo za leo zitahusu kisiwa hicho kinachoonekana.

Hiki ni Kisiwa kidogo mno kipo umbali wa kilometa tatu kutoka fukwe hizo za Spice Beach Kinajulikana kwa jina la Musila, lakini kina historia ya kipekee hapa nchini. Historia ya Kisiwa hiki wakati wa utawala wa wakoloni kilikuwa kikitumika kama Gereza na kwamujibu wa maelezo ya wenyeji hata baada ya uhuru bado kisiwa hiko kiliendelea kutumika kama gereza hadililipojengwa gereza la sasa lililopo Bukoba mjini.

Maajabu ya kisiwa hiki nikwamba kipo nusu kwa maana hukuna uwezekano wowote upande wapili kukaweza kuishi binadamu kwani hakuna kitu kimekatika nusu kwa nusu na upande wapili haupo umebaki ukuta tu.

Lakini jambo lapili la kushangaza nikwamba kuna watu wanaishi wasiozidi 300 na familia zao huku wakilazimisha kupewa huduma zote za kijamii  wakiwa ndani ya sehumu tu ya kisiwa hicho, kwani pamoja na udogo wa kisiwa hicho usiozidi mita 120 urefu na upana mita zisizozidi 50 lakini bado sehemu yenye uwezo wakuishi watu haizidi mita 70.

No comments:

Post a Comment