MAKAMU WA RAIS WA CHINA AWASILI NCHINI
Rais
Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui
Liangyu aliyewasili Ikulu, Dar es Salaam jana, kwa ziara ya kikazi ya
siku tatu nchini.
Makamu Waziri Mkuu Wa China Kuzuru Zanzibar
Na Maelezo Zanzibar 05/09/2012
Makamu Waziri Mkuu wa China Hui Liang anatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho Alkhamis kwa ziara ya siku mbili.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Nchi ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Tanzania,imeeleza kuwa mara tu atakapowasili uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume atapokelewa na Makamu wa Pili
wa Rais Balozi Seif Ali Idd.
Makamu
Waziri Mkuu huyo kwenye uwanja huo atajulishwa na mwenyeji wake kwa
viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo
Mawaziri na pia kuvishwa Shada la Maua na kuangalia ngoma za Utamaduni
wa Zanzibar.
Baadaye
ataelekea Ikulu Zanzibar ambapo atakuwa na mazungumzo na Rais Wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein na
baadaye kutiwa saini makubaliano yatakayoshuhudiwa na Makamo wa Pili wa
Rais Balozi Seif Ali Idd na Makamu Waziri Mkuu huyo wa China.
Usiku
Makamu Waziri Mkuu wa China Hui Liang atahudhuria Chakula cha Usiku
kilichoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais
huko Hotel ya Lagema.
Ijumaa
atatembelea Mji Mkongwe ambapo ataanzia Kanisa la Anglicana Mkunazini
na baadaye Beit el Ajaib na Jumba la Wananchi Forodhani na hatimaye
kuelekea Uwanja wa Ndege kurejea Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment