header

nmb

nmb

Thursday, September 6, 2012

KINGWENDU,RINGO,MTANGA,KITALE WATOKA NA SIMU YA KICHINA


MSANII maarufu wa kazi za sanaa nchini Kitale ameungana na Kampuni ya Bau Entatainment ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa filamu ijulikanayo kama 'Simu ya Kichina' akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema yupo mbioni kutoa filamu hiyo akishilikiana na baadhi ya wasanii wengine maarufu

Kitale Amesema kuwa filamu hiyo itakuwa gumzo jijini kwa kuwa imerekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na kuwashirikisha wasanii waliokomaa kisanii nchini

aliwataja baadhi ya wasanii alioshilikiana nao ni pamoja na Ringo,Kitale mwenyewe,Kingwendu,Mtanga na wengine wengi walioshiriki katika filamu hiyo

aliongeza kwa kusema baadhi ya mafundisho yaliyopo katika filamu hiyo ni Ugumu wa maisha waweza kukupa changamoto ya maisha,ambayo yanaweza kukuletea maendeleo,vilevile ugumu wa maisha waweza sababisha tamaa ambayo yaweza kukupelekea kuwa mwizi katika maisha yako na kukusababishia maisha yako kuwa magumu

filamu hiyo kwa sasa ipo mtaani kwa ajili ya kuwapa wapenzi mbalimbali burudani wakiwa majumbani kwao 'Simu ya Kichina' ni moja ya filamu zenye mafundisho kwa jamii ya kitanzxania hivyo si yakukosa

Bonite Bottlers yawazawadia washindi wa promosheni ya Vuta Mkwanja


 Washindi 16 wa promosheni  ya Vuta mkwanja wakifurahi zawadi ya pesa taslimu waliyo kabidhiwa kiwandani hapo.

 Meneja uzalishaji wa Bonite Bottlers Leonard Mangupili akimkabidhi mshindi Hamid Nkya  mkazi wa Ngaramtoni Arusha ,kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja
Mkuu wa masoko na mauzo wa Bonite Bottlers Christopher Loiruk akimkabidhi mshindi Rahim Hashim mkazi wa Majengo Moshi,  kitita cha shilingi milioni moja alichojishindia kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.

 Mratibu wa mauzo  wa Bonite Bottlers Boniface Mwasi  akimkabidhi mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi laki moja  kwenye promosheni ya Vuta Mkwanja.


Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda cha vinywaji baridi Bonite Bottlers,Christopher Loiruk akizungumza na wanahabari.

*******


Mwandishi Wetu ,Moshi.
KAMPUNI ya vinywaji baridi jamii ya Coca Cola ,Bonite Bottlers jana imekabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa washindi kumi na sita wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambayo inafikia tamati mwezi huu. 

Washindi katika promosheni hiyo iliyoanza mwezi Julai mwaka huu ni pamoja na Fredy Charles ,Hamid Nkya wote wakazi wa Arusha na Rahim Hashim mkazi wa Majengo mjini Moshi ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.

Washindi wengine ni Goodluck Kessy ,Focus Njau ,Joseph Kauwedi,Samson Mushi na Fatuma Ibrahimu ambao walijishindia kaisi cha shilingi laki
moja kila mmoja.  

Mkuu wa masoko na mauzo wa kiwanda hicho Christopher Loiruk aliwataja  washindi wengine waliojishindia kiasi cha shilingi lakini moja kuwa ni Julius Michael,Christina Kessy,Dorin Masawe na Khadijah Said.

Aliwataja washindi wengine ambao wamepatikana katika mikoa ya Arusha,  Kilimnjaro Singida na Manyara kuwa ni  Lucas Sumari ,Magdalena John na Lilian Maro  ambao wote walikabidhiwa fedha zao kiwandani hapo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi ,Loiruk alitoa wito kwa  wateja wa Coca cola kuendelea kunywa kinywaji hicho na jamii yake ili waweze kuibuka washindi wa zawadi mbalimbali ambazo bado zipo katika kinywaji hicho.

“Shindano promosheni imemalizika ,lakini zawadi bado zitaendelea  kutolewa kwa kuwa bado zipo katika mzunguko,kuna washindi ambao wamejishindia zawadi mbalimbali kwa kunywa soda za Coca cola ,Fanta na Sprite …kila soda unayokunywa una nafasi ya kuwa mshindi”alisema Loiruk.

Alisema promosheni hiyo imewezesha wateja wengi wa bidhaa hizo  kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoaja na Sh 1000,000,sh 100,000,10,000,sh 5,000 ,sh 2,000 fulana za Coca cola pamoja na soda ya bure.

Chama Cha Wananchi(CUF)Chazindua Kampeni ya Uchaguzi wa Jimbo la Bububu




 Makamu Mwenyekiti wa CUF Machano Khamis, akimtambulisha Mgombea wa Chama hicho Issa Khamis, kwa Wananchi wa Jimbo la Bububu katika Mkutano wa Uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Skuli Bububu.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akitowa sera za Chama chake kwa  wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya skuli ya bububu jana
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF Machana Khamis, akizinduwa Kampeni za Uchaguzi wa Chama chake katika viwanja vya skuli ya bububu jana
 Mgombea wa Chama cha CUF Issa Khamis akijitambulisha kwa Wananchi wa Jimbo la Bububu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo unaofanyika kutokana na Kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Salim Amuor Mtondoo
 Waheshimiwa wakiwa katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chama cha CUFya Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo.uliozinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa Machano Khamis.
 Waheshimiwa wakiwa katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chama cha CUFya Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo.uliozinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa Machano Khamis.

REDD'S MISS TEMEKE 2012 WAANZA KUJIFUA KUJIANDAA KUWANIA TAJI LA 2012


 Mkufunzi wa warembo katika shoo ya Redd's Miss Temeke, Dickson Daud, akiwanoa warembo hao katika Club ya TCC Chang'ombe jana, tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.
 Warembo wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini jana katika Club ya TCC Chang'ombe , tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.
Warembo wa Redd's Miss Temeke, wakiwa mazoezini jana katika Club ya TCC Chang'ombe , tayari kwa shindano lao litakalofanyika Septemba 21 mwaka huu.
****************************************
JUMLA ya Warembo 15, wa Redd's Miss Temeke, wameanza rasmi kambi yao juzi katika Club ya TCC Chang'ombe tayari kwa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, kumrithi mrembo Husna Twalib anayeshikilia taji hilo la 2011.

Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki hii, chini ya ukufunzi wa Dickson Daud kutoka kikundi cha THT, wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.

Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.

Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Dodoma Wine, gazeti la Jambo Leo, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders na 88.4 Times FM. Warembo wanaendelea na mazoezi na leo, Agosti 5 wanatarajia kutembelewa na Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ambaye pia ni Miss Temeke wa mwaka huo.

Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions
Organizer Miss Temeke 2012

MKURUGENZI WA MAMBO YA NNJE OFISI YA ZANZIBAR AJITAMBULISHA KWA DK.SHEIN.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Zanzibar Balozi Silima K.Haji, aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana  na Mkurugenzui wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Zanzibar Balozi Silima
K. Haji, aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo.

    

KILIMANJARO YAZIPATIA TIMU ZA YANGA NA SIMBA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA LIGI KUU


 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya micheko kwa timu za Yanga na Simba za jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Ilala.Kushoto ni Afisa habari wa timu ya Yanga,Luis Sendeu na kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo kwa Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis Sendeu.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo kwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu.Katikati ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba
Picha ya Pamoja:Toka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu,Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Afisa habari wa Timu ya Yanga,Luis Sendeu.

Zikiwa zimebaki siku tisa kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara 2012/2013, Kilimanjaro Premium Lager imezikabidhi timu za Yanga na Simba vifaa kwa ajili ya michuano hiyo.

Vifaa hivyo vimetolewa ikiwa ni sehemu ya udhamini wa jumla wa dola za Kimarekani milioni 3 (takribani TSh4bilioni) za kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager kwa timu hizo kongwe na zenye ushindani mkubwa na historia yakipee hapa nchini.Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na jezi, kaptula, soksi, vyatu vya mpira, bibs, mipira na mifuko.

KITALE ATOKA NA SIMU YA KICHINA

MSANII maarufu wa kazi za sanaa nchini Kitale ameungana na Kampuni ya Bau Entatainment ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa filamu ijulikanayo kama 'Simu ya Kichina' akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema yupo mbioni kutoa filamu hiyo akishilikiana na baadhi ya wasanii wengine maarufu

Kitale Amesema kuwa filamu hiyo itakuwa gumzo jijini kwa kuwa imerekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na kuwashirikisha wasanii waliokomaa kisanii nchini

aliwataja baadhi ya wasanii alioshilikiana nao ni pamoja na Ringo,Kitale mwenyewe,Kingwendu,Mtanga na wengine wengi walioshiriki katika filamu hiyo

aliongeza kwa kusema baadhi ya mafundisho yaliyopo katika filamu hiyo ni Ugumu wa maisha waweza kukupa changamoto ya maisha,ambayo yanaweza kukuletea maendeleo,vilevile ugumu wa maisha waweza sababisha tamaa ambayo yaweza kukupelekea kuwa mwizi katika maisha yako na kukusababishia maisha yako kuwa magumu

filamu hiyo kwa sasa ipo mtaani kwa ajili ya kuwapa wapenzi mbalimbali burudani wakiwa majumbani kwao 'Simu ya Kichina' ni moja ya filamu zenye mafundisho kwa jamii ya kitanzxania hivyo si yakukosa

TAARAB NA DANSI KURINDIMA DAR LIVE JUMAPILI HII



JAYDEE, DIMPOZ, BANANA, CHEGGE KUIPAMBA REDDS MISS ILALA


Mwandaaji wa shindano hilo atipokua akizungumza na waandishi wa habari.
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Redds Miss Ilala wakiwa kwenye picha ya pamoja tayari kabisa kuingia kwenye fainali itakayofanyika jumamosi hii kwenye ukumbi wa Nyumbani Kinondoni namanga jijini Dar es salaam.

WASANII nguli wa miondoko ya bongofleva sanjari na Machozi Band, kesho watalipamba shindano la kumsaka mrithi wa Salha Israel katika shindano la Miss Ilala litakalofanyika kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge uliopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam.
Wasanii hao ambao watatumia bendi katika kuonesha umahiri wao, wamejumuika kwenye shindano hilo ili kukidhi kile mashabiki wa Miss Ilala wanachotarajia. Mbali ya wasanii hao, msanii wa luninga, Steve Nyerere ndiye atakayeliongoza kama MC ambapo Alhamis(kesho) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye club ya City Sports Lounge kwa ajili ya kutangaza zawadi.
Vimwana 14 wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuwania umalkia wa Kanda ya Manispaa ya Ilala, Redds Miss Ilala 2012, kati yao 12 wiki iliyopita walishindana kwenye kategoria ya kipaji ambapo watano kati yao walitinga hatua ya fainali, ambayo itamaliziwa siku ya shindano lenyewe Ijumaa.
Katika kinyanganyiro hicho mrembo Mary Chizi alikuwa kivutio zaidi kwa jinsi alivyoonesha umahiri wake wa wepesi wa kujvingirisha mwili huku Mectilda Martin akizoa ukumbi mzima kwa kurap na huku akiwa ameandana kwa kucheza hata mavazi yanayotumiwa na wasanii wa miondoko hiyo.
Magdalena Munisi hakuwa nyuma kabisa katika kumwigiza mwanamuziki nguli wa marekani, Ciara kwa umahiri wake wa kulitumia jukwaa, lakini kubwa kuliko pia kwa mrembo Amina Sangawe alibuni nguo kwa kutumia vipande viwili vya khanga ambapo aliliunganisha jukwaani kupitia pini nakumvika mmrembo mwenzie. Stella Moris kwa upande wake alionesha ukali kwa kuimba.
Warembo hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika shoo. 
Miss Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga na inadhaminiwa na City Sports Lounge, Redd's Premmium Cold, Uhuru One, Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, gazeti la Jambo Leo, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM.
Mbali ya walioingia tano bora katika vipaji, warembo wengine wanaoshiriki shindano hilo ni pamoja na Mary Chizi, Matilda Martin, Magdalena Munisi, Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris na Elizaberth Pertty. Wengine ni Wilmina Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.
Mbali ya Redd's Premmiun Cold, wadhamini wengine katika mashindano hayo ni pamoja na Uhuru One, Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na Amaya Salon.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI KUTOKA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)WA KUJADILI UHALIFU WA KIMATAIFA.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema, wakati alipofika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05,2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo Sept 05, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika kuimba wimbo wa Taifa na wakuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema (wa pili kushoto) wakati alipofika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05, 2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema, akisoma hoyuba yake ya ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 -Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Plisi, Inspekta Genarali, Saidi Mwema, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini,

WASANII WA COMEDY


HAWA NDO WAREMBO WATAKAO WANAIA TAJI LA REDD'S MISS NORTHERN ZONE 2012...!!!



Washiriki wa Redds Miss Arusha wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuwasili katika kambi yao ya mazoezi kujiandaa na shindano lao litakalo fanyika Septemba 8, 2012 katika Hoteli ya naura Spring jijini Arusha. Jumla ya waremo 11 wanataraji kucuana vikali kuwania taji hilo. 
(picha na Father Kidevu Blog).

TUNDA MAN ASEMA HATAKI DOGO JANJA ATUMIE CHORUS YAKE WALA KUMTAJA KWENYE NYIMBO ZAKE.


Leo katika Power Jams ya East Africa Radio ,Tunda alifunguka kuhusu Mambo Ya wasanii kutengana na kusema huwa yana leta madhara mengi zaidi kwa pande zote . Kama Dogo janja kuna ngoma anasema ' Na Run Dar City Nikiwa Na JCB ,Na Run Dar City Nikiwa Na Nikiwa na TIP' Na kwa sasa hayupo tena TipTop so maneno kama hayo yapo nje ya uwezo wake na kumfanya apoteze sifa anapokuwa kwenye stage kama Anaposema 'Nipo Na Tunda Man ' Wakati mimi sipo kwenye show hio .Mimi na mshauri asitaje majina hayo sababu maneno kama hayo yana mlostisha na kumpunguzia Credit kwenye stage.
 
Pia kuhusu Dogo Janja kutoa Chorus za Tunda Man kwenye Nyimbo zake ,Tunda amesema jambo kama hilo linawezekana na tumeone wasanii wengi wakifanya hivyo.Beat za nyimbo zipo na sauti zake so ni kitu cha kufanya tu sio issue kubwa sababu huwezi ukasema nipo na TIPTOP Alafu unawatambulisha Watanashati.

USAILI WA MAISHA PLUS 2012 WAENDELEA


Heka heka za Maisha Plus.
 ---
Usaili wa Maisha Plus umeendelea leo (Septemba 4) mkoani Mwanza; baada ya hapa timu nzima itaelekea Morogoro katika wilaya ya Mvomero na siku inayofuata itaibukia Igula, Mkoani Iringa.

"Tukitoka Iringa tunahamia Sumbawanga huko Kantalamba then tutarudi Mbeya, baadaye tutaelekea Kilwa kisha Masasi na Zanzibar itafuatia.

Kaka Bonda akimhoji mshiriki.
---
Dar es Salaam itakuwa ya mwisho ambayo usaili wake utafanyika Septemba 22 na 23," anasema Masoud Kipanya.

Fomu za kushiriki shindano hili kwa Dar es Salaam zinapatikana katika Duka la KP lililopo Millenium Towers Kijitonyama. Kama unahitaji fomu piga namba 0717104303 uelekezwe.
 Mama Shujaa wa Chakula akionyesha ushujaa wa chakula.

Tuesday, September 4, 2012

TIGO YATANGAZA UDHAMINI MKUU WA MAONESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRICA


Mkurugenzi Mtendaji wa Mancom Costantine Magavilla kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo, Alice Maro katikati na Meneja wa Promosheni na Matukio wa Kampuni ya Tigo.Bw. Eduwrd Shilla wakati wa Uzindudhi wa Udhamini wa Maonesho ya Sarakasi ya Mama Africa yatakayoanza Septemba27 mpaka  4 Novemba Picha na www.burudan.blogspot.com

Mkurugenzi Mtendaji wa Mancom Costantine Magavilla kushoto Akisisitiza kitu wakati wa utambulisho wa Udhamini wa Maonesho ya Mama Africa yatakayodhaminiwa na Kampuni ya Tigo picha na www.burudan.blogspot.com
Meneja wa Promosheni na Matukio wa Kampuni ya Tigo.Bw. Eduwrd Shilla katikati akishangaa moja ya watu watakaonesha maonesho ya Mama Africa akiwa nyuma yake

WAUKUMIWA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA KUMUIBIA MWAJILI WAO MILIONI 140

Mpiga Picha wa Global Richard Bukozi kushoto akikimbia sambamba na watuhumiwa wa wizi wa milioni 140 kutoka kwa mwajili wao ambapo wao walikuwa wafanyakazi wa ndani na kukutwa na hatia ya ubadilifu wa fedha hizo katika kezi yao iliyowakabili na kuamliwa kwenda jela miaka mitatu na kutaifishwa kwa nyumba zao walizojenga kutokana na wizi huo
watuhumiwa wa wizi wa milioni 140 kutoka kwa mwajili wao ambapo wao walikuwa wafanyakazi wa ndani na kukutwa na hatia ya ubadilifu wa fedha hizo katika kezi yao iliyowakabili na kuamliwa kwenda jela miaka mitatu na kutaifishwa kwa nyumba zao walizojenga kutokana na wizi huo
Mpiga Picha wa Global Richard Bukozi kushoto akikimbia sambamba na watuhumiwa wa wizi wa milioni 140 kutoka kwa mwajili wao ambapo wao walikuwa wafanyakazi wa ndani na kukutwa na hatia ya ubadilifu wa fedha hizo katika kezi yao iliyowakabili na kuamliwa kwenda jela miaka mitatu na kutaifishwa kwa nyumba zao walizojenga kutokana na wizi huo

No comments:

Post a Comment