
Mastaa wetu wa filamu hapa nchini, wametokelezeaje sasaaa

Wema Sepetu akijiweka sawa.

Wema
Sepetu pia akizungumzia ujio wao ndani ya mji wa Moshi, kuwa wao kama
Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili mkoani humo kusaka vipaji vipya
mbalimbali vya filamu, usahili huo unafanyika kwenye ukumbi wa Mr
Price, ulioko mtaa wa Malindi.

Mmoja
wa wasanii mahiri katika fani ya uigizaji hapa nchini, Wema Sepetu
akifanya mahojiano mafupi na Millard Ayo wa Clouds FM mapema leo kwenye
amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo linafanyika jioni ya
leo mpaka lyamba ndani ya uwanja wa chuo cha Ushirika,ndani ya mji wa
Moshi, ambapo katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni nusu
mnyama tu a.k.a 5,000/= kwa kila kichwa.

Msanii
mwingine nyota katika tasnia ya filamu, Aunt Ezekiel akielezea ni
namna tamasha la Serengeti Fiesta lilivyowambamba wakazi wa mji wa
Moshi na vitongoji vyake, na pia ujio wao kuwatafuta wasanii wapya
chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikikua siku hadi siku.


Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya mji wa Moshi

Jacob
Steven a.k.a Steven akifafanua jambo mapema leo mtaa wa Malindi
kuhusiana na suala zima la wasanii hao kulivamia jiji la Moshi.


Wema na Steve Nyerere Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.

Kiongozi wa msafara wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Mully B akiwa
na mastaa wa filamu, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama
kawa.

Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.

Pichani
ni Gari aina ya Vits itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2012, kwa mshindi atakaejishindia kwenye droo
itakayofanyika katika uwanja wa chuo cha ushirika, ambako tamasha hilo
litarindima mpaka majogoo.

Mtangazaji
wa Clouds FM,Millard Ayo akiwa Live mapema leo mtaa wa Malindi katika
mpango mzima wa amsha amsha kwa wakazi wa Moshi kuhusiana na tamasha la
Serengeti Fiesta 2012, ambapo pia katika tamasha hilo kutatolewa
zawadi mbalimbali ikiwemo gari ndogo aina ya Vits kama uinavyo pichani
ikinadiwa vilivyo.

Kawa
kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa
magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka
kampuni ya GAPCO ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment