Watuhumiwa waliokamatwa kwa kutaka kumuua Albino waachiwa Huru!!
WATUHUMIWA watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kujaribu kumuua Mtoto Mlemavu wa Ngozi Albino Adam Robaert (13) katika mahakama ya wilaya ya Geita, wameachiwa huru na sasa wamerejea nyumbani wakiendelea na maisha yao ya kawaida.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa haari hii, watuhumiwa hao wakiwemo wazazi wa Mtoto huyo Robert Tangawizi, waliachiwa huru tangu Mei 30 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi kutokana na amri kutoka kwa Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali Elieza Feleshi.
Watuhumiwa walioachiwa huru kwa amri hiyo ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa serikali ni pamoja na Baba wa Mlemavu huyo Robert Tangawizi,Mama wa Kambo Agnes Majala,pamoja na mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji Machibya Alphonce wote wakazi wa kijiji cha Nyaruguguna kata Tarafa na Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.
Washitakiwa hao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka mawili kila mmoja katika mahakama hiyo ya wilaya,ambayo ni pamoja na Kujaribu kuua,pamoja na kula njama ya kutaka kuua,ambapo walikamatwa Oktoba mwaka 2011 na baada ya mahojiano na polisi walifikishwa katika mahakama hiyo ya wilaya.
Inadaiwa kuwa kukamatwa kwa watuhumkiwa hao kulitokana na maelezo ya mtoto mmelavu aliyejeruhiwa ambaye alidai kuwa siku ya tukio baba yake mzazi alimkaribisha mtuhumiwa anayedaiwa kumkata na kumjeruhi pamoja na kwamba mtoto huyo tayari alikuwa amekwishatoa taarifa za mtuhumiwa huyo kwamba alikuwa akimfuatilia machungani na kumdanganyadanganya.

No comments:
Post a Comment