Kaimu
Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein
Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake
leo Malindi Mjini Zanzibar-Picha na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar
--
26/07/2012
Mamlaka
ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi
Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo
kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo. Aidha meli hizo
zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika
maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa
Meli hizo.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini
Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama
Zanzibar. Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha
na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya
Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za
kufanyia kazi meli hizo.
Amefahamisha
kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na
uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara
katika safari zao. Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri
na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka
Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa
abiria.
No comments:
Post a Comment