header

nmb

nmb

Tuesday, July 24, 2012

MAISHA NI KUSAIDIANA

 
You might al

MAMBO YA RUNGWE HAYA!!!!!!!



 
 Wachezaji wa Yanga na Mafunzo wakimpepea Juma Mmanga baada ya kuzimia katika mechi ya robo fainali ya kuwania Kombe la Kagame, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Mchezaji huyo aligongana na mchezaji Yanga katika harakati za kuwania mpira. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)

 Msalaba mwenkundi na madakatari wa timu ya Mafunzo wakitoa msaada kwa mchezaji huyo.
                                      Wachezaji wakiwa  wamepigwa butwaa
                                     Akipelekwa kwenye ambulance tayari kukimbizwa hospitali kwa matibabu
  Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw Salum Mwalim akiwaelezea wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kutoka kushoto Abbas Mtemvu (Temeke),David Silinde (Mbozi Magharibi) na Mussa Azan (Ilala) faida za kujiunga na huduma za mkataba za kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifurahia huduma za Vodacom wakati kampuni hiyo ilipowahudumia wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wiki iliyopita. Wa tatu kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kati Said Arfi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kati , Said Arfi na Mbunge wa Viti Maalum, Agripina Buyogela, Kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma July 23,2012.Picha naOfisiya Waziri Mkuu

Dk Rotich kufungua mafunzo ya Wapigapicha kesho Arusha


NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich (pichani) anataraji kufungua mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yatakayo anza Julai 23-26, 2012 mjini Arusha.

Juma la wapigapicha 10 kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki wanataraji kuhudhuria mafunzo hayo ya siku tatu ya Upigaji yatakayofanyika katika Hotel mjini Arusha.

Mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jumuia ya Afrika Mashariki na Shirika la Kijerumani (EAC) na  GIZ yatahusiha wapigapicha hao kumi, wawili kutoka kila nchi.

Tanzania inawakilishwa na Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti na Habari za Mtandao, Mroki Mroki, Mwasisi na Mhariri Mkuu wa FATHER KIDEVU BLOG pamoja na Mwandshi wa Kampuni ya Mwanachi Comunication mjini Arusha, Filbert Rweyemamu.

Tayari wapigapicha hao wa Habari wapo mkoani Arusha wakiwasubiri wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuwasili kwa kuanza mafunzo hayo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ni Balozi wa Heshima wa Utalii nchini Kenya na Mwenyekiti wa mfuko wa 50 Treasures of  Kenya, Hartmut Fiebig.Chanzo Father Kidevu Blog
 

 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akiongea na waandishi wa habari Katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga kufanikisha sherehe za  maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya mnazi mmoja leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa.
Askari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa mabalozi wan chi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania  Balozi Ibrahim Mukubi kutoka  Uganda akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya siku ya mashujaa itakayofanyika tarehe 25, Julai 2012.


Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
   Dar es salaam.
 
Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya  Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012  jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
 
Amesema katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es  salaam  baadhi ya barabara  zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
 
Aidha Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
 
“ Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu”

Rais Kikwete afuturu na Viongozi wa Dini Mbeya

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali aliowaalika katika futari katika ikulu ya mjini Mbeya jana jioni.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya magharibi muda mfupi kabla ya futari ambayo aliwaalika viongozi mbalimbali wa dini mjini Mbeya jana(Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya magharibi muda mfupi kabla ya futari ambayo aliwaalika viongozi mbalimbali wa dini mjini Mbeya jana(Picha n
 
Mchezaji Nadir Haroub (kulia) wa Yanga akipiga mpira huku Jaku Juma wa Mafunzo ya Zanzibar akiruka katika mechi ya robo fainali ya kuwania Kombe la Kagame, jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Mafinzo ya Zanzibar, wakishangilia bao la kuongoza dhidi ya Yanga

                                Kelvin Yondani wa Yanga akiruka kuokoa hatari dhidi ya timu ya Mafunzo

 

Rais Kikwete azindua mradi wa maji Mbeya

 Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya nchini Cerian Philberto Sebregondi(kushoto),Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji safi na mazingira Mjini Mbeya leo mchana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa JumANNE Maghembe  wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira mjni humo leo mcha

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya akutana na Spika Makinda


   Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni mlezi wa Hospitali ya CCBRT Mhe. Anne Makinda akisalimiana na  Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Mhe. Jose Manuel Barroso alipowasili Hospitalini hapo jana kujionea shughuli za Hospitali hiyo. Serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya umekuwa ukiichangia fedha nyingi hospitali hiyo.
  Rais Barosso akisaini kitabu cha wageni.
Wagonjwa waliotibiwa na kupona fistula.

Mpango wa Upanuzi wa Hospitali ya CCBRT
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi akimuelezea jambo Rais wa Kamisheni ya Ulaya 
Spika wa Bunge mama Anne Makinda na uongozi wa CCBRT Wakimuaga kiongozi huyo.
Picha ya pamoja

MKUTANO WA CCM MJINI KIGOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI,) Aggrey Mwanri akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye  Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini  Kigoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye  Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini  Kigoma.
Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Mahusiano, Steven Wasira akihutubia kwenye  mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye  Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini  Kigoma.
Mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa CCM katika Uwanja wa Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma
Wazee kwenye mkutano wa CCM, Uwanjwa wa Community Cetre Mwanga Kigoma
Viongozi mbalimbali wa CCM waliohudhuria katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment