header

nmb

nmb

Thursday, July 5, 2012

JK AKUTANA NA VIONGOZI WA TAHLISO

Thursday, July 5, 2012
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa Umoja wa  Wanafunzi wa  Vyuo vya Elimu ya Juu  nchini (TAHLISO) walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam siku ya jana, Julai 4, 2012. Viongozi hao walikuwa wakihudhuria kongamano la mabadiliko ya katiba lililokuwa linafanyika katika ukumbi wa Karimjee.
 

MZEE MWINYI AKABIDHI MA-TREKTA KWA WAKULIMA WA KWADELO, WILAYA YA KONDOA

 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassani Mwinyi akimkabidhi funguo za trekta, Mwenyekiti wa Kijiji  cha Makilinya, Siraji Abdallah Mahingu, wakati wa Mwinyi alipokabidhi trekta tatu kwa wakulima wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, leo, nyumbani kwake, Msasani, Dar es Salaam. Kushoto kwa Mzee Mwinyi ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati aliyefanikisha upatikanaji wa trekta hizo.
 Rais mstaafu, Ali Hassani Mwinyi akiijaribu trekta wakati wa makabidhiano hayo. Kushoto ni Diwani Kariati
 Mzee Mwinyi akiwa na wazee wa CCM kutoka Kata hiyo waliofika katika makabidhiano ya trekta hizo.
 Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na ugeni huo
Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliofika nyumbani kwake wakati wa makabidhiano hayo.
 Blogger wenu Bashir Nkoromo, naye akapata fursa ya kumsalimia Mzee Mwinyi
 Diwani Omari Kariati na Wazee aliofika nao, wakipata chai na Mzee Mwinyi
Mzee Mwinyi, Kushoto akipata chai na wageni wake

No comments:

Post a Comment