header

nmb

nmb

Thursday, June 21, 2012

Mama aibiwa mtoto

Mwanamke Bi.Modesta Sumbuko ( 26) mkazi wa kijiji cha Butende , kata ya Mpunze
wilayani Kahama  akiwa na majonzi ya kuibiwa mtoto wake mchanga  wa kiume wa
siku tatu aliyeibiwa kwenye  wodi ya wazazi katika hospitari ya Wilaya ya
Kahama  alikokuwa amejifungua kwa njia ya upasuaji , kichanga hicho kilibiwa juzi
saa 11 alfajiri  na mama mmoja asiyefahamika , juu pichani  akiwa amekaa kwenye kitanda
chake ndani ya wodi hiyo. 
 
Na Mpiga Picha Wetu 

WABUNGE wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Simba na Yanga wanatarajia kucheza mechi ya aina yake Julai 7 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Lengo la mechi hiyo ni kuwakutanisha watanzania kuwa kitu kimoja pamoja na kuchangia mfuko wa elimu kwa asilimia 20 ya mapato yatakayopatikana siku hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari jana jijini dar es Salaam Mratibu wa mechi hiyo Juma Mbizo ambaye pia ni mkurugenzi wa ukumbi wa  Dar Live alisema, wameamua kufanya tamasha hilo ili kuisaidia serikali  kujenga mabweni ya shule kwa upande wa wasichana hapa nchini.

"Tamasha hilo litakuwa la aina yake hasa pale tutakapowaona waheshimiwa wakichuana kwa lengo la kubadilishana mawazo ya nchi kujua wapi walipo na tunapokwenda,"Alisema Mbizo.

Aliwataka wadau mbali mbali wa soka kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushuhudia viwango vitakavyoonyeshwa na wabunge hao.

Alisema,wadau hao wajiokeze ili kushuhudia upinzani utakaonyeshwa uwanjani badala ya kusikia kupitia vyombo vya habari.

Mbali na mechi hiyo vile vile kutakuwa na pambano la ngumi ambalo litawakutanisha mabondia  Cheka na Kaseba,BOngo Muvi na Bongo Fleva,pamoja na burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya Chameleon (Uganda) na Diamond.
 

BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact, inatarajia kutoa burudani kwa mashabiki wa timu ya Chelsea, nchini katika kuisherehekea kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la FA itakayofanyika Jumapili Msasani Beach Club, Dar es Salaam.

Mbali na bendi hiyo, wasanii mbalimbali akiwemo Shilole, Mr. Nice, Muumin Mwinjuma, Chaz Baba na Irene Uwoya watakuwepo siku hiyo kunogesha sherehe hizo.

WAZIRI APENDEKEZA UMISSETA KUUNDWA TWIGA STARS B


WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenela Mukangara amesema Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) ya mwaka huu yatatumika kuunda timu ya pili ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika juzi mjini Kibaha, Waziri Fenela alisema haina budi kuunda timu B ya wanawake kwa kutumia wachezaji watakaopatikana katika michuano hiyo.

Makabidhiano ya Faru toka Uingereza



No comments:

Post a Comment