header

nmb

nmb

Tuesday, May 15, 2012

UWABA yahamasisha wananchi kupanda baiskeli

Baadhi ya wapanda baiskeli katika matembezaji ya uhamasishaji upandaji wa baiskeli kama vyombo vingine vya usafiri, wakijitayarisha kupanda baiskeli zao zao kwa ajili ya matembezi hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, kuelekea viwanja vya Biafra, Kinondoni na kurudi tena kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Matembezi hayo yaliandaliwa na Umoja wa Wapanda baiskeli Tanzania (UWABA) na kushirikisha watu wa rika mbalimbali. (Picha zote na Khamisi Mussa)


Waendesha baiskeli inayoendeshwa na watu wawili, Jeremy Yamin (mbele) na Alicia Yamin, wakiwa tayari kwa matembezi hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.


Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akisalimiana na Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi (kushoto), wakati wa kuanza kwa matembezi hayo, yaliyokuwa yakihamasisha wananchi kupanda chombo hicho kwa ajili ya kuimarisha afya zao kimazoezi.



Mgeni rasmi katika matembezi ya baiskeli, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (wa pili kulia), akiwa Balozi wa Wapanda baiskeli duniani, Filberto Sebregondi (wa pili kushoto) pamoja na wapanda baiskeli wengine, wakiendesha baiskeli zao hizo kuelekea viwanja vya Biafra Kinondoni na kisha kurudi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.

No comments:

Post a Comment