Makamu Mkuu Shule ya Sekondari Kivesa, Faustine Mrosso, shule hiyo iliyopo Kata ya Chanika inahudumia vijiji vya Kwediyamba, Kwedizando na Kwekambara maeneo ambayo ni mbali na shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Komnyang'anyo wakitembea barabarani kuelekea kwenye makazi yao vijiji mbalimbali vinavyoizunguka shule hiyo.
WANANCHI wilayani Handeni wameilalamikia mazingira magumu kimiundombinu ya shule za sekondari za kata katika wilaya hilo na kudai ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi na kukatisha masomo.
Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti katika mahojiano ya baadhi ya wakazi wa Handeni na mwandishi wa habari hizi ndani ya uchunguzi uliofanywa hivi karibuni maeneo anuai ya wilaya hiyo kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA).
Abdulah Mwamponda Mkazi wa Kijiji cha Msasa, wilayani Handeni alisema shule nyingi za kata zimejengwa mbali na makazi ya wanafunzi jambo ambalo linawapa mzigo wazazi na wanafunzi kujitafutia usafiri wa kwenda na kurudi shuleni.
Alisema katika kijiji hicho wapo wanafunzi ambao hutembea umbali wa kilometa 12 na hata 20 kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kwenda na kurudi shuleni, umbali ambao umekuwa na vishawishi vingi hasa kwa wanafunzi wa kike kiusafiri.
Alisema usafiri katika vijiji hivyo ni wa baiskeli na pikipiki (bodaboda) ambao wazazi wengi wanashindwa kugharamia hivyo watoto kutembea kwa umbali huo, huku wakati mwingine wakishawishika kupewa msaada wa lifti na madereva wa bodaboda ambao baadaye huanza kushirikiana nao kimapenzi.
Mzazi Fatuma Shaban kutoka Kijiji cha Komnyang’anyo alisema wanafunzi wengi huondoka nyumbani kwao saa 10 za asubuhi na kurudi usiku kutokana na umbali huo huku wengine wakishinda shuleni bila chochote kutokana na uduni wa maisha ya kaya nyingi eneo hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani, Rajab Nyange alisema katika shule hiyo iliyopo Kata ya Vibaoni nje kidogo ya Mji wa Handeni wapo wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali takribani kilimeta sita hadi 10 kutoka nyumbani kwao, ambao hutembea kilomita 20 kila siku yaani kwenda na kurudi shuleni jambo ambalo linaibua vishawishi kwa wanafunzi.
“Mzazi anashindwa hata kumpa mtoto wake sh. 100 au 200 kila siku ya shule kwa ajili ya kula chochote awapo shuleni, je ataweza kumlipia mtoto huyo gharama za usafiri ambazo ni za juu zaidi kutokana na umbali kutoka kijiji kimoja hadi kingine,” alihoji Nyange.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Hassan Mwachibuzi anasema Ofisi yake haina taarifa za ubakaji wa moja kwa moja japokuwa anakiri kuwepo kwa vitendo vya utoro kwa wanafunzi wote kwa sababu mbalimbali. Anasema pamoja na hayo utoro waweza kuingiliana na ukatishwaji masomo kwa mimba.
Kiongozi huyu anakiri suala la umbali wa shule huchangia vishawishi kadhaa vya wanafunzi hasa wa kike kukumbwa na vikwazo kadhaa katika masomo yao. Hata hivyo anabainisha kuwa uongozi unajitahidi kulitatua suala hilo kwa kuongeza ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi katika shule za kata ili wanafunzi waondokane na vikwavyo anuai.
Aliongeza kuwa tayari wamejenga hosteli katika maeneo ya Kisasa, Kwamsisi, Misima, na kudai kuwa wanaendelea maeneo mengine kwa kushirikiana na wananchi na wahisani huku lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na hosteli zake kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali na shule.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Sunday, May 13, 2012
AL AHLY SHANDY YASHINDA PENATI 9-8 NA KUITOA MASHINDANONI SIMBA HUKO SUDAN
Tayari timu ya Simba iko uwanjani hivi sasa ikipambana na timu ya Al Ahly Shandy ya huko Shandy nchini Sudan katika kipindi cha dakika 90 Simba imefungwa magoli matatu wakati yenyewe haijapata kitu, mchezo huo ulianza saa mbili kamili kwa majira ya Tanzania.
Baada ya kuamriwa kupigwa penati kwa kanuni za mashindano hayo.
Timu ya Al Ahly Shandy imeshinda penati 9-8 dhindi timu ya Simba na kuisukumiza nje ya mashindano.
Baada ya kuamriwa kupigwa penati kwa kanuni za mashindano hayo.
Timu ya Al Ahly Shandy imeshinda penati 9-8 dhindi timu ya Simba na kuisukumiza nje ya mashindano.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrka (CAF) vizur.
Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo.
Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo.
muandishi: JOHN BUKUKU
MANCHESTER CITY HAVE WON THE PREMIER LEAGUE!!!
MANCHESTER CITY HAVE WON THE PREMIER LEAGUE!!! The final whistle blows and the fans are on the pitch!
90 min+5: Everyone's happy. QPR will stay up because Bolton haven't won at Stoke.
GOAL!!!!!! Manchester City 3-2 QPR (Aguero, 90 min+4): Sergio Aguero has won the Premier League title for Manchester City! Balotelli made a nuisance of himself on the edge of the area, the ball ran free on the edge of the area, Aguero bursted on to it and as QPR defenders collapsed around him, he smashed it past Paddy Kenny from eight yards out! Michael Thomas, eat your heart out.
90 min+3: Two minutes. Manchester United have done their bit: they've won 1-0.;
IT'S ON! Manchester City 2-2 QPR (Dzeko, 90 min+2): Edin Dzeko powers a header past Kenny from close range from Silva's corner. Manchester City need one goal to win the title. They have three minutes.
90 min+1: From the third corner, Balotelli meets it from six yards out and Kenny wonderfully claws it out. He then catches the second corner. He;'s more than made up for his error that led to Zabaleta's goal. Again it looked like he had to score. There will be five minutes more of this. City need two goals.
90 min: Balotelli twists and turns and shoots, but it's deflected wide by the superb Onuoha. Corner to City. Another corner to City. Another corner to City.
muandishi: JOHN BUKUKU
HALMASHAURI KUU YA CCM YAKUTANA DODOMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya
Mrisho Kikwete (kulia)akiendesha semina ya Viongozi wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa,iliyofanyika katika ukumbi wa White House,Makao Makuu ya
Chama Hicho Mjini Dodoma jana,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM Dk.Ali Mohamed Shein,na (katikati) Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid
Karume.[Picha na Ofisi ya Rais Zanzibar.]
Mrisho Kikwete (kulia)akiendesha semina ya Viongozi wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa,iliyofanyika katika ukumbi wa White House,Makao Makuu ya
Chama Hicho Mjini Dodoma jana,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM Dk.Ali Mohamed Shein,na (katikati) Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid
Karume.[Picha na Ofisi ya Rais Zanzibar.]
SIKU MOJA BAADA YA KUPOKELEWA KAMA MFALME ,KANISA LA ASKOFU KAKOBE LAMFANYIA MAOMBI MBUNGE FILIKUNJOMBE
SIKU moja baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kupokelewa jimboni na wapiga kura wake kama mfalme Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(F.G.B.F) linaloongoza na askofu Zacharia Kakobe wilayani Ludewa lamfanyia maombi maalum .
Huku mwenyewe akiahidi kuendelea kupambana na Vitendo vya ufisadi kwa Taifa bila kuogopa na kuwaomba Waumini wa Kanisa hilo na madhehebu mengine pamoja na wapiga kura wake wote kuzidi kumwombea zaidi Kwani kazi iliyopo mbele yake ya kupambana na ufisadi ni nzito yahitaji maombi.
Kanisa hilo limfanyia mbunge Filikunjombe maombi hayo jana katika ibada maalum ambayo iliandaliwa na uongozi wa Kanisa hilo kama njia ya kuungana na vyama vya siasa na wananchi wa jimbo hilo kuutambua mchango na kazi nzito ya mbunge huyo katika kupambana na vitendo vya ufisadi nchini.
Katika maombi idaba hiyo Mchungaji wa Kanisa hilo Faustin Sambilanda.
alisema kuwa kazi ilinayofanywa na Filikunjombe katika kulipigania Taifa ni kubwa na hivyo kila mtanzania na kila kiongozi wa dini wanaowajibu wa kuendelea kumwombea mbunge huyo na wengine ambao wapo kwa maslahi ya watanzania .
muandishi: JOHN BUKUKU
MWILI WA MPIAGAJI RACHEL MWILIGWA UTAAGWA LEO UBUNGO
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinawajulisha wadau mbalimbali kuwa mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania Rachel Mwiligwa utaagwa kesho Jumatatu Mei 14, 2012 saa nne kamili asubuhi Kanisa la Anglikana Ubungo, ambalo lipo nyuma ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msemaji wa familia, Alex Chimila, taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitaanza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 6:00 mchana, tayari kwa msafara wa kwenda kuzika katika Makaburi ya Tegeta A, Goba, jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa kuaga mwili kwenye eneo hilo una lengo la kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa ya kushiriki kwenye tukio hilo.
Tunawaomba waandishi wa habari za michezo na wadau wengine wa michezo na burudani kujitokeza kwa wingi asubuhi kwenda kumuaga mpendwa wetu. Rachel alikumbwa na mauti usiku wa kuamkia juzi kwenye hospitali ya Mwananyamla, Dar es Salaam.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA




No comments:
Post a Comment