header

nmb

nmb

Tuesday, March 6, 2012

WAANDISHI IRINGA WATUMIA MANDAMANO KUDAI HAKI


Maandamano ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa yamesababisha baadhi ya wananchi kusitisha shughuli zao na kushiriki maandamano hayo.

Mwandishi wa habari aliyeko Iringa amesema maandamano hayo yaliyopita mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa likiwemo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoni ambako mwandishi huyo anasema wasafiri walishuka katika mabasi walimokuwa kwa ajili ya kuanza safari na kuungana na wanahabari hao kwa kusindikiza kwa muda maandamano hayo .

Wakitoa maoni yao juu ya maandamano hayo baadhi ya wananchi wakiwemo Maneno Mbuma na mzee Said Sanga walisema kuwa hofu ya mkuu wa mkoa wa Iringa kupokea maandamano hayo haikupaswa kuwepo kutokana na utulivu na hekima ya hali ya juu iliyoonyeshwa na wanahabari hao.

Mbuma alisema kuwa jamii ya mkoa wa Iringa haipotayari kuendelea kukosa haki yao ya msingi ya kupata habari kwa ubaguzi na manyanyaso ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa dhidi ya wanahabari na kuwa vyombo vyote vya habari vinapaswa kupewa haki sawa ya kuhabarisha umma juu ya matukio yanayotokea katika mkoa.

Hivyo alisema kama kweli ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa haikuwa na matatizo hayo ambayo wanahabari wameamua kuyapinga basi mkuu wa mkoa Dkt Christina Ishengoma angekubali kupokea maandamano hayo ya amani ila kukimbia kupokea maandamano hayo ni sawa na kuogopa ukweli dhidi ya ofisi yake.

Akipokea maandamano hayo ambayo kwa mujibu wa mwandishi wa habari hiyo walikuwa zaidi ya 60 wa vyombo mbali mbali mkoani Iringa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC) ambao ndio walidhamini maandamano hayo,Daud Mwangosi alisema kuwa wengi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment