KLABU ya soka ya Simba imetishia kugomea kucheza mechi zake katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, pia kuzuia wanachama wake kuingia uwanjani, kutokana na uonevu wanaofanyiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika mchakato mzima wa mapato ya mlangoni.
Hatua hiyo inafuatia juzi TFF kuikata Simba mgao wake wote wa shilingi mil.3.5 ilioupata kupitia mapato ya mchezo wao wa ligi kuu baina yao na Kagera Sugar ya Kagera kwa madai ya fidia ya shilingi mil.tano wanazotakiwa kulipa baada ya wanaodaiwa mashabiki wa Simba kuharibu viti vya uwanja huo katika mechi baina ya Simba na Kiyovu iliyofanyika jumapili iliyopita.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo kwamba wanashangazwa na uonevu wa wazi unaofanywa na TFF , kwa kuwa uwanja huo si mali yao na wamekuwa wakilipa fedha nyingi kabla ya mchezo kama tahadhari kwa uharibifu wowote utakaotokea lakini haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.
“Mfano mechi yetu na Kagera Sugar juzi mapato yalikuwa mil.24 na baada ya makato ya mamlaka mbalimbali zilibaki mil.7 na vilabu kugawana hivyo kila timu kupata mil.3.5, huu ni unyonyaji kabisa kwani pamoja na vilabu kugharamika kwa fedha nyingi kwenye maandalizi lakini mwisho wa siku wanakuja kufaidika watu wasiochangia mapato yoyote,”Alisema Kwa habari zaidi tembelea :http://mamapipiro.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment