header

nmb

nmb

Tuesday, February 21, 2012

Wanaume kenya mhuuuuuu






Wanaume wanaoishi ndani ya ardhi ya 254 Kenya, baada ya mateso ya muda mrefu, mateso ambayo kesi zake zinaongezeka kila siku, wamtangaza msimamo wao mpya wa kugoma kwa siku sita kula msosi nyumbani kwao, msosi uliopikwa na wake zao kama ishara ya kukataa wake zao kuendelea kuwapiga ambapo sasa watakua wanajisevia msosi hotelini.

Mwenyekiti wa Chama cha maendeleo ya Kina baba Nderitu Njoka, amefunguka kwamba huo mgomo ni wa kuwataka wanawake kuacha kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.

Kwa mujibu wa NTV, Nderitu alikua akiamplfy huo msimamo wakati akiwa kwenye hospitali kuu ya mji wa Nakuru Rift valley ambako kulikua na mwanaume mmoja alielazwa kuugulia maumivu yaliyotokana na kipigo cha mke wake, kipigo ambacho alipewa nyumbani kwake, ambapo kabla ya kupewa kipigo mke wake alimuita kama vile mtoto mdogo anaecheza nje na mama anataka aingie ndani, baada ya hapo akamfungia chumbani na kumpa kifinyo.

Mwenyekiti wa chama cha maendeleo ya kina baba, Nderitu Njoka amethibitisha kwamba mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopewa kifinyo na wake zao ambapo idadi ya waliopewa hicho kifinyo mpaka sasa inakaribia nusu milioni.

Pamoja na adhabu za kifinyo, wanaume wengine pia wamekua wakinyimwa haki yao ya ndoa ambapo kwa Nairobi wanaume wanaopewa kifinyo hicho ni laki tatu.






No comments:

Post a Comment