header

nmb

nmb

Tuesday, February 21, 2012

KIDUM, LINEX, KHADIJA KOPA, SIKINDE NA ‘KINA RIHANNA’ WAKOLEZA MOTO DAR LIVEMOTO mkali uliendelea kuwaka kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar usiku wa kuamkia leo ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo: Linex, Khadija Kopa, Alex Machejo, na makundi ya ngoma za asili ya Machozi na Mawazo Group, bendi ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Dogo Lila na msanii Kidum kutoka nchini Burundi, wote hao walikamua sambamba na washiriki wa shindano la ‘Vaa, Imba na Cheza,Kama Rihanna’ na kuufanya umati mkubwa ulifoka hapo kupata burudani isiyopimika katika hali yoyote.


Wasanii hao walitumbuiza kwenye Family Day Bonanza ambalo hufanyika kila siku ya Jumapili chini ya usimamizi wa uongozi wa kituo hicho cha Dar Live kilichopo Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam


Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

Pichani ni msanii kutoka nchini Burundi, Jean Pierre ‘Kidum’, akikamua na mmoja wa wasanii wa Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, aliyekuwa mshereheshaji wa bonanza la Dar Live huko Mbagala jijini Dar es salaam..

Akimshikia maiki mmoja wa wapiga vyombo wake.


Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Sunday Mangu ‘Linex’, akitumbuiza.

Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa, akiwajibika.

Baadhi ya ‘Kina Rihanna’ walioingia 12 Bora wakiwa katika pozi.

Walivyowatoa udenda mashabiki.

Shabiki akilimaindi jukwaa alipopewa fursa ya kuonyesha machejo.
Sehemu ya umati uliofurika kituoni hapo

No comments:

Post a Comment