header

nmb

nmb

Tuesday, February 7, 2012

DAR LIVE Ilivyo teka wakazi wa Dar


MASHABIKI waliohudhuria burudani katika kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam walipata starehe ya kutosha kutoka kwa wanamuziki Juma Kassim ‘Sir Nature’ wa hapa nchini, na Namelesa kutoka Kenya ambapo walitoa makamuzi ya nguvu usiku wa kuamkia leo.


Wanamuziki hao walitoa kauli za kuushukuru umati mkubwa uliojitokeza kwenye onyesho hilo wakisema hawakutegemea Mbagala kuwa na mashabiki wa burudani wengi hivyo.Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mashauzi Classic Band, Wakali Dancers, Zuhura na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya huku washiriki wa shindano la “Cheza, Vaa Imba Kama Rihanna” wakitambulishwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo. Kama anavyoonekana jukwaani mwanamuziki Nameless akitumbuiza na mmoja wa mashabiki aliyemwita apande jukwaani. Wadau wa Dar Live Wakiwa kwenye pozi la pamoja.

Wanenguaji na wanamuziki wa FM Academia wakionyesha uwezo wa nyonga zao.

Kundi zima la Wanaume Halisi likiwajibika jukwaani.

Kiongozi wa Mashauzi Classic Band, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, akinengua na mpiga gitaa wake.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Zuhura, akipagawisha mashabiki.

Mwanamuziki Ambwene Yesayah ‘AY’, akiwasalimia mashabiki..Chanzo;Fullshangwe Blog

No comments:

Post a Comment