Dave akiibusu maiti ya aliyekuwa mchumba wake.
MKURUGENZI wa kituo kiumoja cha televisheni nchini Thiland aitwaye Chadil Deffy au Deff Yingyuen, akitaka kuonyesha upendo wake kwa mchumba wake wa siku nyingi aliyekuwa akiitwa Sarinya au “Anne” Kamsook, aliyefariki hivikaribuni kwa ajali ya gari, aliamua kufunga ndoa na marehemu huyo.

Baada ya kufanya hivyo, alizituma picha za tukio hilo kwenye mtandao wa Facebook na YouTube, kitendo ambacho kiliwashangaza watu wengi duniani.
Ndoa hiyo ya ajabu ilifanyika wakati mmoja na mazishi ya marehemu bi.harusi huko Amphur Muang, jimbo la Surin, nchini Thailand ambapo pia palifanyika mazishi ya mchumba huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 sehemu hiyo hiyo.
Deffy ambaye jina lake la utani ni “Dave” alikutana na Sarinya wakati wanasoma Chuo Kikuu cha Asia Mashariki miaka kumi iliyopita na wakapanga kuoana, lakini mwanamke huyo akafariki Januari 3 mwaka huu.
Wakati wa mazishi hayo, bwana harusi alionekana akiwa amevalia suti nyeusi na akimvisha mchumba wake huyo pete.
Tukio hilo lilihudhuliwa na ndugu,marafiki na jamaa wengi wakiwemo wacheza sinema, waimbaji na wanafunzi wenzao wa chuo kikuu hicho ambao walisoma nao

No comments:
Post a Comment