header

nmb

nmb

Wednesday, January 4, 2012

MAADHIMISHO YA MIAKA 48 YA MAPINDUZI YA ZAZNIBAR ZINAANZA LEO!!









Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar .Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa ratiba ya sherehe za kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinaanza rasmi leo katika majimbo yote 50 ya Unguja na Pemba .Katibu wa Kamati ya Sherehe hizo Dk. Khalid Mohamed amesema kuanzia leo kutakuwa na kazi ya usafishaji mazingira katika majimbo yote 50 ya Zanzibar ambapo wasimamizi wa zoezi hilo ni Halimashauri za Wilaya, Baraza la Manispaa,Mabaraza ya Miji na Masheha. Kwa mujibu wa Ratiba hiyo inaonesha kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein atazindua Jengo la Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi .Aidha Rais Shein anatarajiwa pia kuzindua Barabara ya Dunga-Amani katika hafala itakayofanyika huko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Januari 9 atafungua barabara mbili (2) za Wilaya ya Chake Chake Pemba ambazo ni Chanjamjawiri-Tundaua na Chanjamjawiri-Pujini.Katika hatua nyingine Rais Shein anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Nyumba ya Madaktari kutoka Norway katika Chuo cha Afya cha Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi .Halikakadhalika Rais Shein atafungua Barabara nne (4) za Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba ikiwemo Mtambile-Kengeja, Mtambile-Kangani, Mizingani-Wambaa na Kenya-Chambani .Shughuli nyengine atakazofanya Dk.Shein ni Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi huko Weni Mkoa wa Kaskazini Pemba na ataendesha zoezi la kuchangia Mfuko wa Fedha za Mikopo (Fund Rising) katika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar .Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim seif Sharif Hamad anatarajiwa kuzindua Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Mfuko wa Barabara Zanzibar ambapo jioni yake atafungua Jengo la Idara ya Uvuvi liliopo Maruhubi katika Mkoa wa Mjini Magharibi .Aidha Maalim seif Sharif Hamad atafungua Tangi la Maji Gongoni Wilaya ya Micheweni Pemba ikiwa ni shamra sharma za kutimiza mika 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Naye Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba ambapo pia atafungua Soko la Jumapili (Sunday Market) kwa wajasiriamali liliopo Michenzani Mkoa wa Mjini Magharibi .

No comments:

Post a Comment