header

nmb

nmb

Wednesday, January 25, 2012

KITCHEN PARTY GALA KUFANYIKA JANUARI 28, 2011
Waandaaji wa Kitchen Party Gala, Dina Marious (kushoto) akiwa na Vida Mahimbo walipokutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam kuzungumzia Kitchen party gala.Tukio ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Danken house mikocheni ambao ndiyo ukumbi rasmi wa shughuli hii jumamosi ya tarehe 28 january.


Wasichana na wanawake wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea kushindwa kusimama katika mahusiano yao. Teknolojia, mwamko wa elimu,wanawake kumiliki biashara binafsi, kazi, wazazi hawahusishwi, kila mtu mjuaji, kujisahau n.k


Matokeo yake talaka nyingi na mahusiano kuvunjika sasa tunataka kumkumbusha mwanamke wajibu wake na nafasi yake katika mahusiano. Ajitambue.


Msimu wa piliEneo hili limelenga kukuza ujuzi wa mwanamke katika Nyanja za kijamii zaidi. Kupitia eneo hili mwanamke atajifunza mambo mbalimbali kiasili na kisasa ambayo mwanamke anaengia au aliyeko au anaetegemea kuingia katika mahusiano na ndoa. Mambo kama malezi ya watoto, nafasi yake katika jamii umuhimu kujiamini na mengineyo.


Wazo hili limekuja mara baada ya kuona kwamba ule muda wanawake wanaopata kuongea mambo haya kwenye kitchen party ni mchache na hautoshi kumfahamisha mwanamke mambo yote muhimu. Mambo ambayo ni lazima ayajue au hata kama anayajua kutokana na pilika pilika za maisha anajisahau.Tukio hili kufanyika jumamosi hii ya tarehe 28 January 2012. Kuanzia saa nane mchana mpaka saa mbili usiku katika ukumbi wa Danken house uliopo mikocheni kwa warioba.
Watoa mada ni watu wenye uwezo katika swala zima la uelimishaji.Aunt sadaka; Ni mwana saikolojia aliyebobea katika maswala ya wanawake na watoto.Ana uwezo katika Nyanja hii ambao umetokana kielimi na uzoefu wa kukutana na kesi mbalimbali amabazo zinazo mguza mwanamke hivyo kuweza kuwa funzo kwa wengine.
Bi Chau: Ni mwanamke ambaye mbali na kuwa katika fani ya sanaa kwa muda mrefu wamekua wakito amafunzo kwa wanawake tokea muda mrefu. Mafunzo ya mahusiano, ndoa na familia kwa ujumla.
Mama Victor; Ni mtumishi wa Mungu katika dini ya kikristo ambaye anaelimisha wanawake kwa mafunzo ya kidini. Anafundisha mwanamke kujitambua vile mungu amempa uwezo wa kuitumikia jamii yake kama mlezi na kiongozi.
Kwa ufupi hawa ndio wakufunzi katika tukio letu hili la women in Balance jumamosi hii katika msimu wa pili.Burudani itatolewa na Nyota Waziri.
Huu ni mkakati wa mwaka mzima huu 2012 na tutakutana kila mwezi mpaka mwezi march ambapo ratiba itabadilika na wanaume kuhusishwa.WADHAMINI WETU WA SIKU HII NI BAILEYS (kinywaji), MGen Insuarance, Cocacola, Cooperate Image na Clouds Fm.
IMETOLEWA NA MRATIBU WA WOMEN IN BALANCE.

No comments:

Post a Comment