header

nmb

nmb

Tuesday, January 17, 2012

Khadija Kopa, Tip Top Connection wafunika Dar Live!Moto wa Dar Live unazidi kupamba moto kila wiki na wikiendi iliyopita, mwimbaji taarab mahiri nchini Khadija Kopa akiwa na TOT pamoja na wasanii wa Tip Top Connection, wakiongozwa na Rais wao Madee, walitoa shoo kali ya kufa mtu na kuacha historia ya kipekee kwa wakazi wa wilaya ya Temeke na kwingineko waliohudhuria shoo hiyo. Picha zinaonesha sehemu ya mpango mzima ulivyokuwa:(Picha kwa hisani ya Full Shangwe Blog)

Mashabiki wakijiachia ndani ya Dar Live.

Kiongozi wa Tip Top Connection Madee akipagawisha mashabiki wa Mbagala

Mkata nyonga mahiri wa TOT taarab, Queen Emmy akifanya vitu vyake jukwaani

Safu ya unenguaji ya TOT ikiongozwa na Khadija Kopa jukwaani.

Ndani ya kiwanja cha Dar Live mashabiki wakila bata.

Watoto wakijiachia ndani ya Dar Live .Na Mwaikenda

No comments:

Post a Comment