header

nmb

nmb

Wednesday, January 4, 2012

JAMBAZI LAUA POLISI ARUSHA, LAMJERUHI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI.







KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA SHANGARAI

KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia baada ya kupigwa risasi ya shingoni na mkuu wa upelezi wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya Baada ya kupigwa Risasi ya Begani na jambazi sugu mkoani hapa ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mapema jana jioni kamanda wa polisi mkoa wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana alfajiri majira ya saakumi.

.

Kamanda Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mara baada ya askari hao kupata taarifa t

oka kwa wasamaria wema na kwenda kwa ajili ya upekuzi katika nyumba ya Bi.Agness Silas ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajili ya makazi ya majambazi mjini hapa.

Alibainisha kuwa mara baada ya askari hao kufika katika nyuma hiyo waligonga hodi na kufunguliwa mrango na askari hao kuingia ndani kwa bahati mbaya jambazi hendry alikuwa amejipanga vizuri na kuanza kuwashambulia kwa lisasi mfululizo ambazo moja ilimpata askari huyo shingoni na kusababisha kifo chake na kumjerui Mrakibu huyo wa wilaya ya Arusha vijijini.


Alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi waliendelea na msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo ilikuwa inasadikiwa kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za ujambazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Alitaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya Short gun ,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi za kuvaa usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika shuguli mbalimbali za uhalifu.

Bw.Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao ni Daines Msawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi.

Aidha mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya majmbazi hayo yaliyokimbia

No comments:

Post a Comment