header

nmb

nmb

Monday, January 9, 2012

Dkt Slaa kuhutubia Jijini Mbeya.Nyomi kama hii inatarajiwa!!







Katibu Mkuuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Dkt.Wilbroad Slaa anatarajia kutua Jijini Mbeya Januari 12 kwa ziara ya kuhamasisha chama mkoani humo.

Kwa mujibuwa taarifa ya Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya Eddo Makatta anasema kuwa Dkt.Slaa ataingia Jijini Mbeya na kufanya mikutano ya ndani kisha mikutano yahadhara katika maeneo mbalimbali ya wazi.

Makattaalisema kuwa ziara hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho kukutana na wapigakura wake kwa nia ya ,kuwazindua juu ya mambo mbalimbali ya hujuma na ufisadidhidi ya wananchi unaofanywa viongozi waliopo madarakani.

Alisema kuwa ziara ya Dkt. Slaa inakuja wakatikukiwa na mijadala na midahalo mbalimbali inayoendelea juu ya marekebisho yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano.

No comments:

Post a Comment