header

nmb

nmb

Wednesday, January 4, 2012

Baada ya James Alex Msekela kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia sasa kuapishwa januari 5!!









Katika taarifa yake, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue amesema kuwa Rais Kikwete amemteua Dkt. James Alex Msekela kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.



Kabla ya hapo Mheshimiwa Msekela alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.



Aidha, taarifa hiyo ya Bwana Sefue imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Bwana Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Naibu Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.



Kabla ya hapo, Bwana Mwinyi alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.



Katibu Mkuu kiongozi amesema katika taarifa yake kuwa wateuliwa hao wawili wataapishwa keshokutwa, Alhamisi, Januari 5, 2012.



Imetolewa na:



Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment