Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo, nchini India, kwa takriban miezi minane, amerejea nchini, baada ya afya yake kuimarika. Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Gerson Lwenge, Profesa Mwandosya alirejea nchini juzi. Mwingine aliyethibitisha jana kurejea kwa waziri huyo mwandamizi, ni mkewe, Lucy Mwandosya. Hata hivyo, Mhandisi Lwenge, ambaye alizungumza na jana, alipotakiwa kueleza maendeleo ya afya ya Waziri Mwandosya, alijibu: “Sijamuona, ndio naenda. Ukinitafuta baadaye nitakwambia.” Awali, Mhandisi Lwenge, alipoulizwa kama Waziri Mwandosya amerejea nchini, alijibu: “Ndio amerudi” na alipotakiwa kueleza lini alirejea, alijibu: “Jana (juzi).” Baadaye, majira ya saa 11.05 jioni jana, ilimtafuta Profesa Mwandosya kwa simu yake ya mkononi, ambayo ilipokelewa na mkewe, Lucy. Baada ya mwandishi kujitambulisha na kueleza shida yake ya kutaka kuzungumza na Profesa Mwandosya, Lucy, alisema muda huo waziri asingeweza kuzungumza kwa vile alikuwa anapumzika.
No comments:
Post a Comment