header

nmb

nmb

Thursday, December 22, 2011

Mkuu wa nchi atuma Rambirambi kwa waliopoteza maisha na kuwasihi walio okoka kuwa na subira!!




RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa

Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea jana, Jumanne, Desemba 20, 2011.


Aidha, Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu.



Rais Kikwete pia ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.



Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: "Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar es Salaam tokea jana.



Amesema: "Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote."



Ameongeza Rais Kikwete: "Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wotwalioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu.


"Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.








Mkazi wa Mwananyamala Kisiwani ambaye ameshindwa kuvumilia na kuiacha nyumba yake na kuokoa maisha yake baada ya kuona maji yanazidi kuongezeka Jijini Dar es Salaam




Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Haroub akitafakari nini cha kufanya wakati akiwatembelea waathirika wa mafuriko katika eneo lake la Mwananyamala Kisiwani Jijini Dar es Salaam
Diwani akiwa amembeba kijana wakati wa mafuriko hayo akiambatana na wakazi wa eneo hilo Mwananyamala Kisiwani


Mkazi wa Mwananyamala Kisiwani akitafakari bila majibu kama TASAF,walitoa mamilioni ya pesa zikichanganywa na michango ya wakazi wa Mwananyamala kuwa zote zimepotea bure kwani maji yamesha bomoa na kutengeneza njia nyingine tena kama inavyoonekana



Mafuriko ni hatari yanabeba hadi nyoka




Duh bonge la nyoka




Mkazi wa Mwananyamala Kisiwani maarufu kwa jina la Rajaburajabu akijaribu kuzuia vitu vya ndani visibebwe na maji wakati wa mafuriko yalilolikumba Jiji la Dar es Salaam
Hapa amekata tamaa sasa lakini hana pa kwenda na vitu vyake hana pa kupeleka kaamua itavyokuwa na iwe wakati huofamilia yake wamekaa juu kidogokawatoandani




Hii ndio hali halisi Maji yanaingia mpaka madirishani




Hali si shwali watu wameyakimbia makaziyao



Siondoki bora nife




Mkazi wa Mwananyamala kavumila mwisho kaona atakufa kaamua kuikimbia nyumba yake




Watu wakiyakimbia makazi yao




Watu wakiyakimbia makazi yao baada ya kuona maji yanazidi kuongezeka




Binti huyu akingoja kuokolewa akishuka katika kigogo hichi tu maji yalikuwa yakimzidi kimo




Watu wakiondoka kwenye makazi yao wengine wanakwenda kuwasaidia watu

No comments:

Post a Comment