header

nmb

nmb

Wednesday, December 21, 2011

Maafa Dar Walio kaidi kuhama Mabondeni wengi wapoteza maisha kwa Mafuriko,Tabata, Jangwani na Magomeni.Pia familia yawatu 9 wafamaji


Haya ni baadhi tu kati ya maeneo yaliyojaa maji yatokanayo na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, hapa ni maeneo ya kati ya Tabata na Buguruni, kama picha hii inavyoonyesha nyumba zikiwa zimefunikwa na kuelea majini leo hii.Eneo hili ni sehemu unapopita Mto Msimbazi ambao umeharibu madaraja kadhaa yanayounganisha eneo moja na jingine.


Haya ni maeneo ya Vingunguti kuelekea Tabata, eneo la Viwanda.













Mvua zinazoendelea kunyesha zimeendelea kuleta maafa makubwa baada ya watu wapatao 9 wa familia moja eneo la mto wa Kigogo jijini Dar es Salaam pamoja na mtu mmoja ambaye alidhaniwa ni teja alifuta tairi la gari ambalo aliliona kwenye maji na kuzama mpaka sasa hali ni mbaya eneo hilo na faya wamekuwa wakiendelea kuwatafuta watu hao bila mafanikio.

Mpaka sasa hali si hali katika maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam ambapo Mbezi Beach maeneo ya Bondeni daraja limevunjika upande na kusababisha magari kushindwa kuingia mjini.


Hapa ni katika Daraja la Kawe eneo la Bondeni linapojengwa Daraja jipya tayari pakiwa pameshazuiliwa kupita kutokana na daraja hilo kuweka nyufa za kukatika kwa daraja hilo ambalo maji yamelizidia na kupita juu.

Kingo za Daraja hilo zikiwa tayari zimebomoka kutokana na kuzidiwa nguvu na maji hayo ya mvua kubwa iliyonyesha leo.

Baadhi ya abiria wakitembea kwa miguu baada ya eneo hilo njia kufungwa na kuzuiliwa kutopita magari baada ya maji kujaa na kupita juu ya Daraja.


Uwanja wa Ndege pia katika Maegesho ya Ndege ndogo asubuhi ya leo ulikuwa umejaa maji, lakini ndege ziliweza kuendelea na safari zake kama kawaida.(Picha kwa Hisani ya Sufiani mafoto)

No comments:

Post a Comment