Na Emmanuel M. Kimweri wa Fullshangwe- Dar es salaam
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) leo limetoa msaada wa vyakula wenye thamani ya zaidi shilingi million ishirini na tano (million 25) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mh. Said Meck Sadiq kama sehemu ya mchango wao kwa wananchi walioathirika wa mafuriko hasa wale waliopo katika vituo maalum vya jijini Dar es Salaam.
Akikabithi msaada huo Brigedia Jenerali Cylil Ivor Mhaiki kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, alisema hii ni sehemu ya msaada kwa wananchi ambao wamekumbwa na mafuriko kwa maeneo mengi ya jijini Dar es Salaam na kuahidi kuwa Jeshi la Wananchi litashirikiana kusaidia wananchi.
“Kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na penda kuwapa pole wale wote waliokumbwa na mafuriko yaliyo sababishwa na mvua zilizo nyesha siku chache zilizopita na kupelekea kusababisha vifo na upotevu wa mali kwa wananchi”, alisema
Jeshi la wananchi linatambua wakati mgumu unao wakabili wananchi ambao wamekumbwa na mafuriko na kwa msaada huo tunaokabidhi kwa mkuu wa mkoa ni sehemu ya msaada ambao jeshi limetoa kwa wananchi waathirika, msaada huo ni Mchele kilo 75,000 ni sawa na gunia 75, Maharage kilo 1600 ni sawa na maguni 16, Sukari kilo 1600 ni sawa na gunia 16 na Majani ya chai kilogram 224.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadiq alisema anayo furaha kwa wananchi na taasisi mabilimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuendelea kuisaidi wananchi wenzetu ambao wamekumbwa na mafuriko na kukosa hifadhi na kulazimika kuishi katika vituo maalumu.
“Kwa niaba ya serikali napenda kutoa shukrani za dhati kwa JWTZ kwa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko yaliyo ikumba nchi yetu na kusababisha watu kupoteza maisha na wengi wao kukosa makazi ya kuishi na upotevu wa mali zao” alisema
Pia alimweleza Brigedia Jenerali Cylil Ivor Mhaiki kuwa serikali tayari imeshafanya tathimini ya kuwagawia viwanja wale wote ambao manaishi mabondeni.
“Nachukua fulsa hii kwa kuwajulisha wananchi kuwa tunatambua huduma muhimu za mwanadamu hivyo katika sehemu zote tulizo fanya uthamini wa kugawa viwanja tumetenga maeneo ya Shule, Barabara, vituo vya huduma za afya sambamba na kupeleka umeme maeneo hayo ili kupisha shughuli za kimaendeleo” alisema
No comments:
Post a Comment