MWANADADA anayekuja juu katika tasnia ya filamu Bongo Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amelalamikia muongozaji aliyejulikana kwa jina moja tu la Karim kwa kudhulumu filamu ya watayarishaji kutoka Lushoto Jijini Tanga na kutumia jina lake la Shilole kama ndiyo jina la filamu hiyo, Jambo ambalo Shilole anaona kuigizwa mjini na muongozaji wa filamu hiyo, kwa kutumia jina lake bila mapatano ya aina yoyote, kwani yeye aliingia mkataba wa kuigiza na si jina lake kutumika katika filamu hiyo
Akiongea na FC Shilole anasema kuwa yeye aliitwa kushiriki filamu kama muigizaji, kwa hiyo baada ya kumalizika ile filamu yeye akiwa kama msanii alijua kuwa tayari amemaliza kazi yake kama muigizaji wala hakuwa anafikiri kama kuna siku watu watakuja kumlalamikia kwa kuhusika na utapeli wa aina yoyote, kama ilivyotokea katika filamu hiyo iliyopewa jina lake la shilole bila ridhaa yake, hata hivyo anasema kuwa Karim hakumshirikisha kwa jambo lolote kuhusu matumizi ya jina hilo, jambo ambalo Shilole anasema limemkera sana hata kufikia kufuta namba ya simu ya Karimu katika simu yake.
“Namshanga sana huyu kijana Karim kwa kutumia jina langu katika filamu isiyonihusu kabisa, lakini mbaya zaidi kufanya jambo hilo bila woga wala kunishirikisha au hata kunijulisha tu, kuwa ametumia jina langu katika filamu hiyo, nashangaa wale watayarishaji wanakuja kunituhumu mimi kama nimeshiriki katika dhuluma wakati mimi sijui chochote kuhusu filamu hiyo, Karim kanikera sana,” analonga Shilole.
Na FC
Haitoshi kufuta nomba ya sim ya huyo promota dada kama nikweli hamja ogea kuhusu jinalako kutumika nenda KOSOTA au njoo Prhabari tukusaidie
No comments:
Post a Comment