Mh. John Mnyika Mbunge wa Jimbo la Ubungo Dar es salaam.
Kuna taarifa saa hizi zimetufikia kupitia kipindi cha Redio ya Clouds FM cha Leo tena, kuhusu shule moja ya Msingi Jimbo la Ubungo.
Shule ya Msingi Tuliani iliyopo katika Kata ya Kilungule Wilaya ya Kinondoni kuna vitendo vichafu vinaendelea kufanywa na Vijana wahuni wa maeneo hayo vya kuwalawiti wanafunzi wa Shule hiyo ya Tuliani.
Vitendo hivyo mpaka walimu wanavijua na wanashindwa la kufanya kwa sababu nao Walimu wa kike wanaogopa wanaweza kubakwa. Vitendo hivyo hufanywa na vijana hao katika vyoo vya shule hiyo, kutokana na hali ilivyo mbaya mpaka walimu pia wakienda Chooni ni lazima wasindikizane kwa kuwaogopa Wabakaji hao. Kwa taarifa pia kupitia Leo tena, Polisi wa kituo cha jirani wanalijua hili lakini hawalifanyii kazi.
No comments:
Post a Comment