Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.
Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.
Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?
Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.

No comments:
Post a Comment