Rais wa zamani wa Libya Muhammar Gaddafi.
Nitatia shaka kama viongozi wote wa Bara la Afrika kama walimuelewa wakati anaonyesha picha hizi wakati Taifa lake likiwa limevamiwa na Waasi wakishirikiana na majeshi ya NATO.
Ni matarajio yangu ningesikia kiongozi ata mmoja wa kiafrika akihoji hili la kuangushwa utawala wa Gaddafi, kwa bahati mbaya hakuna kiongozi hata mmoja aliyehoji hili mpaka Bendera ya waasi ikapandisha, kuashiria ndani ya UN utawala wa Gaddafi ndio mwisho.
Mimi binafsi naamini kama kungekuwa na viongozi kama Kwame Nkhrumah, Nelson Mandela, Mwl. Julius Nyerer,e Hyle se las, Martin Luther King, Malkom X, Samora Machel na wengine wengi wapenda haki, kama kikao hiki cha 66 cha UN kingekalika.
Tunaona Israel Waziri Mkuu wao anavyoonyesha ujasiri kwenye mambo ya Waisrael nampongeza sana, ameonyesha uzalendo kwa wananchi wake.
No comments:
Post a Comment