Balozi Huyo aliyasema hayo katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye ofisi za Balozi huyo zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es salaam, mwandishi wa habari hii alitaka kufahamu maandalizi ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda , anayetarajiwa kufanya ziara ya siku SITA Nchini BRAZIL kuanzia mwanzoni mwa Mwezi ujao.
Akizungumzia suala la Rasilimali watu, aliishauri Serikali kuanzisha vyuo AU Kushirikiana na vyuo vikuu vitakavyotoa elimu ya juu katika kuwezesha kutoa wahitimu wenye sifa za kufanya kazi katika sekta za Nishati akitolea mfano shughuli itakayohitaji wahandisi wengi wa uchimbaji mafuta katika kipindi kijacho.
Kuhusu Safari ya Mheshimiwa waziri Mkuu,Balozi LUZ amesema, Katika ziara hiyo mheshimiwa waziri anatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kuvutia na yatakayoleta tija kwa nchi ya Tanzania, zikiwemo sekta za kilimo kwasababu kilimo Kwanza ndiyo kipaumbele cha nchi, pia atatembelea maeneo ya mifugo, Miundombinu pamoja na miradi ya mbalimbali ya maendeleo nchini humo sambamba na kukutana na wafanyabishara wenye nia ya kuwekeza Tanzania na muungano wa vyama mbalimbali.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu PINDA , ataongozana na msafara wa Viongozi kadhaa kutoka hapa nchini Akiwemo waziri wa Nishati na Madini Bw.William Ngeleja, Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu pamoja na viongozi wengine wa juu wa serikali .
No comments:
Post a Comment