Jina lake kamili ni Omary Muba, mwanamuziki mwenye Ndoto ya kumfikia oliva mutukuzi, safari yake ikimuziki ilianza since 2001 walipoamua kuunda kundi lijulikanalo kama FDC lililojumuisha wasanii mbalimbali akiwemo Pig Black na wengineo
walifanikiwa kurekodi nyimbo moja ilifahamika kwa jina la Kindumbwendumbwe enzi za Mika Mwamba ndani ya Fm Studio.
2007 aliibuka tena kama solo artist baada ya kuona wasanii wengi chipukizi wanafanya vizuri na wanatoka katika ulimwengu huo.
Aliibuka na ngoma moja iliyofahamika kama rudi mwana ambayo alimshirikisha D knob hiyo ilimpaisha na kupata nafasi ya kuongeza nyingine.
2008 mwishoni aliwaacha mashabiki midomo wazi ambapo alifanya shoo kubwa MJini Mombasa ambayo iliweza kumkutanisha na msanii Dullayo na kufanikiwa kuunda kundi lililojulikana kama Makavu Live linalojumuisha wasanii wengi.
Ndani ya Makavu Live kila msanii anaruhusiwa kufanya kazi yake binafsi kwa lengo la kujitangaza zaidi kwa mashabiki, akiwa ndani ya kundi hilo Kundi hilo ameweza kutoa ngoma nyingi kama vile Ongea mwanangu, maneno wapi ambayo ilikuwa ina hadhi ya mnanda na Sikiliza mchumba alimshirikisha dullayo.
Kwa sasa OMmy G ameamua kubadili aina ya Musiki na kuchanganya kwa kutumia staili ya utamaduni na kuingiza ubunifu mpya wa kisasa.
Wambembele ndio nyimbo iliyoitambulisha style hii mpya ya muziki aliyoamua kuitumia kwa sasa. Na mungu si Athumani ilifanikiwa kushika chart kama moto unavosambaa kwenye nyaya za umeme.
Ilianza kuingia kwenye chati bora katika vipindi mbali mbali vya redio na Televisheni pamoja na magazetini hapo ndipo alianza kupata moyo wa kuendelea na muziki..
Matarajio yake ni kufuata nyayo za mwanamuziki OLiva Mutukuzi pamoja na za Mwidini Ngurumo.
No comments:
Post a Comment