header

nmb

nmb

Wednesday, December 22, 2010

TDL KUZALISHA NA KUZA MIVINYO YA IMAGI WINE INAYO TENGENEZWA NA MALIGHAFI YA ZABIBU YA HAPA NCHINUI

Meneja Mkuu wa TDL (KONYAGI) Mr Davir Mgwasa akifafanua jambo

Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL) leo imezindua mivinyo yake mipya kabisa ya DODOMA and IMAGI ikiwa ni nyongeza katika idadi ya mivinyo inayozalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo ndani ya na nje ya Tanzania.
Meneja ,asoko wa KONYAGI Joseph Chibehe (wa pili kulia) akiwa na wafanyakazi wezake katika uzinduzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi huo jijini Dar es salaam Meneja vinywaji wa TDL Bi Matha Bangu alisema mivinyo iliyokuwa ikizalishwa awali na kampuni hiyo ilikuwa katika rangi mbili tofauti za dry white na Red na hii iliyozinduliwa leo zitakuwa katika muonekano na rangi tatu ambazo ni Natural sweet,red na white.

Alisema mvinyo wa Overmeer ambao ni moja kati ya mivinyo ya TDL imejipatia umaarufu mkubwa kwa watumiaji wanotumia mvinyo huo ambapo wameipokea ladha yake nzuri na kufurahia upatikanaji wake kwenye muundo wa boksi linaloweza kubebwa katika sherehe na shuguli mbali mbali.

Bi Bangu alisema kuanzia mwaka 2006 kampuni ya Tanzania Distilleries imekuwa ikitumia zao la zabibu linalozalishwa mkoani Dodoma kwaajili ya kutengeneza na kufanikisha mvinyo wa Overmeer kuwa wa kwanza miongoni mwa mivinyo innozaliwa kwa kiwango cha kimataifa nchini Tanzania na kupelekea mkoa wa Dodoma kuwa kitovu cha upatikanaji na uzalishaji wa mivinyo nchini Tanzania

Aidha aliongeza kwamba kuzinduliwa kwa mivinyo ya Dodoma na Imagi ni kielelezo tosha cha kuonyesha juhudi za kampuni ya Tanzania Distilleries za kusaidia kilimo na kuboresha maisha ya wakulima wa Nyanja zote yaani wakulima wadogo ,wakati na wakubwa lakini pia kuunga mkono kauli mbiu ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kuhamasisha mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo chini ya kauli mbiu isemayo “Kilimo kwanza”
Gadna na mkewe pia walikuwepo
Kwa upande wake Meneja mauzo wa TDL bwana Joseph Chibehe alisema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha linasaidia wakulima katika kupata mbegu bora za mmea wa Zabibu na kutaza namna ya kuwapatia mafuzo mazuri juu ya kilimo cha zao hilo”TDL itatazama namna ya kuwasaidia wakulima wa zao la zabibu kwa kuwapatia mafunzo yatakayopelekea kuongeza uzalishaji wa zao la Zabibu na hatimae waweze kuongeza kipato chao ,lakini pia kuweza kuongeza fursa za kujipatia ajira ndani ya mkoa wa Dodoma kupitia kilimo cha Zabibibu “alisema Bwana Chibehe.

Alisema tayari wakulima wa ndani wameshapata nafasi ya kupatiwa mafunzo ya kilimo cha zao hilo toka kwa wataaalam toka nchini Afrika ya Kusini ambapo katika mafuzo hayo wameweza kijipatia mbinu mbalimbali juu ya kilimo cha kisasa cha Zabibu.

Alisema mivinyo ya Dodoma na Image inatoa nafasi ya uchaguzi kwa wanywaji wa mivinyo kuweza kuwa na chagua la aina ya mvinyo apendao kunywa ikiwa ni pamoja na

-White wine kwa wale wanaopendelea kunywa wine wanapokula kuku,samaki au tambi.

-Red wine yenye ladha nzuri na inafaa unapotumia nyama ya kuchoma,kukaanga au chakula chenye viungo.

-Natural wine inayoendana vizuri na ulaji wa mboga za majani au mlo mwepesi wakati wowote.

Alimalizia kwa kusema kwamba kampuni ya TDL inafurahi sana kuwapa wateja wake fursa ya kufurahia wine hizi katika ladha mbalimbali. Pia TDL inajivunia kuiweka Tanzania katika orodha ya nchi mojawapo zinazotengeneza wine yenye hadhi ya kimataifa.
Habari kwa hisani ya Michuzi

No comments:

Post a Comment