header

nmb

nmb

Tuesday, November 2, 2010

Shedr Shein ashinda kiti cha urais zanzibar aahidi makubwa!!



MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM, DK. ALI MOHAMED SHEIN (PICHANI) AMESHINDA URAIS WA ZANZIBAR KWA MUJIBU WA MATOKEO YA TUME YA UCHAGUZI YALIYOTANGAZWA S HIVI PUNDE ,AMBAPO DR. SHEIN AMEWEZA KUIBUKA MSHINDI KWA ASILIMIA 66.4%

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AMEYAKUBALI MATOKEO NA KUIPONGEZA CCM NA MGOMBEA WAKE. AKIHUTUBIA HIVI PUNDE MAALIM SEIF AMEMKUBALI DK. ALI MOHAMED SHEIN KWA KUPATA RIDHAA YA WAZANZIBARI KUWAONGOZA KWA MIAKA 5 IJAYO.

HATA HIVYO MAALIM SEIF AMESEMA KUNA DOSARI ZINAZOTOKANA NA BAADHI YA MAOFISA NA KUMUOMBA RAIS MTEULE KUWA MWANGALIFU NA HILO ILI NCHI ISIFIKE PABAYA.

AMESEMA KATIKA UCHAGUZI HUU HAKUNA MSHINDI AMA MSHINDWA. MSHINDI NI MZANZIBARI. NA KAMUOMBA RAIS MTEULE AHAKIKISHE HILO ILI HALI YA HEWA ISIJE KUCHAFUKA.

MAALIM SEIF AMEMALIZA KUTOA HOTUBA YAKE NA KWENDA NA KWENDA KUMPA MKONO DK. SHEIN HUKU VIFIJO NA NDEREMO VIKIIBUKA KATIKA
Zitto Kabwe kwa tiketi ya CHADEMA amelitetea jimbo lake la Kigoma Kaskazini

Kwa mujibu ya Matokeo rasmi yaliyotangazwa na wasimamizi wa vituo hivi /husika ni kwamba katika jimbo la Kigoma Mjini mgombea Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha CCM,Bwa Peter Serukamba amembwaga mpinzani wake wa chama cha CHADEMA ,Bwa.Ali Mlee kwa kuibuka na kura 20,594 kwa 19,414.

Wakati huo huo mgombea Ubunge kwa jimbo la Kigoma Kaskazini,Bwa.Zitto Kabwe amemgaragaza mgombea mwenzake wa chama cha CCM,Bw.Robbinson Lembo,ambapo Zitto Kabwe ameibuka na kura 23,500 huku Robbinson akiibuka na kura 18,970.

Kama vile haitoshi huko jijini Mwanza katika jimbo la Ilemela,matokeo rasmi ni kwamba Mgombea wa chama cha CHADEMA,Hyness Willson amembwaga vibaya mgombea wa chama cha CCM,Bwa.Antony Diallo kwa kujinyakulia kura zaidi ya 30,000 dhidi ya Diallo ambaye amepata kura 26870.Nae Bw.Lawlence Masha wa CCM amebwagwa kwa namna ya pekee na mpinzani wake wa CHADEMA Bw.Ezekia Wenje kwa kuibuka na kura 38,131 huku Masha akipata kura 27,883.
KILE KILICHOITWA MATUMAINI MAPYA KWA ZANZIBAR.Za blog ya jiachie

No comments:

Post a Comment