Magari aina ya Huyndai I10 yanayotolewa kwa washindi wa shindano la Shinda Mkoko linaloendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania yakipita chini ya bango la kampuni hiyo lenye ujumbe Habari ndiyo hii katika makutano ya barabara za Kawawa na Uhuru ya Ilala Boma leo. Miongoni mwa magari hayo yapatayo 30 ambayo yamehifadhiwa katika ghala la kampuni ya kuuza magari ya FK Motors leo yalipitishwa katika maeneo mbalimbali jijini ili kuwaonyesha wananchi juu ya uhakika wa shindano hilo la Shinda Mkoko kutoka Vodacom Tanzania ambalo linaendeshwa kila siku na mshindi kujishinda gari moja la Hyundai I10 kila siku. Jumla ya magari matatu yameshatolewa kwa washindi wa shindano hilo kutoka mkoani Dar es salaam, Dodoma na Ruvuma na magari mengine yataendelea kutolewa kwa washindi kwa utaratibu uliopangwa na Vodacom Tanzania ambapo kwa sasa taratibu mbalimbali za usajili wa magari hayo zinaendelea.(Habari na picha kwa hisani ya full shangwe)
No comments:
Post a Comment