header

nmb

nmb

Tuesday, October 12, 2010

MWANAFUNZI ALIYE BAKWA NA KUDUNGWA MIMBA, AENDA AFUNGWA , KISA KAMTETEA MBAKAJIWAKE!!

NA DEGE MASOLI,Handeni
Mahakama ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela miaka miwili mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Konje, Joyce Mganga (15) kwa kosa la kumtetea kijana aliyembaka na kumpa ujauzito.

Mbele ya Mahakama hiyo Septemba 16, mwaka huu, Joyce alijikuta hatiani kwa kile kilichoelezwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Patrick Maligana kuwa alishindwa kuisaidia mahakama dhidi ya kijana Mbaraka Abdallah anayetuhumiwa kwa ubakaji.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Brown Lupembe, kesi ya msingi ilikuwa ni tuhuma za msichana huyo kubakwa na kupewa ujauzito, hivyo kufika kwake mbele ya chombo hicho cha sheria ilikuwa ni kutoa ushahidi wa tukio hilo.

Joyce Mganga (15).
Hata hivyo, Joyce anadaiwa kumkera hakimu pale aliposema: “Simfahamu Abdallah (kijana anayetuhumiwa kumbaka) wala sijawahi kumuona.”

Kauli hiyo ilitafsiriwa na mahakama kuwa ni njama za makusudi za mwanafunzi huyo kupindisha ukweli kwa lengo la kumtetea mtuhumiwa.

Miguno na taharuki iliibuka ghafla mahakamani hapo pale hakimu alipoamuru msichana huyo mwenye ujauzito wa miezi sita kuwekwa rumande na siku nne baadaye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki nne.


Hapa ndiyo nyumbani kwao mwananfunzi aliyefungwa jela baada ya kupewa mimba.

Kutokana na hukumu hiyo kufanyika bila wazazi wa mwanafunzi huyo kuwepo mahakamani, Joyce alishindwa kulipa faini hiyo na kupelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo, huku kesi ya msingi ikipangwa kusikilizwa Oktoba 12, mwaka huu.

Ukurasa wa hukumu hiyo ulipofungwa, gazeti hili lilianza harakati za kuwatafuta wazazi wa mwanafunzi huyo ambapo Mwandishi Wetu alisafiri mpaka Kijiji cha Kwabaya wilayani Handeni alikokuwa akiishi Joyce na familia yake.

Mbali ya kujionea mazingira magumu aliyokuwa akiishi mwanafunzi huyo na familia yake, mpekua habari wetu alifanikiwa kuzungumza na baba wa msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mhina.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA GAZETI LA UWAZI

No comments:

Post a Comment