TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa nchini kuzingatia Amani na Utulivu katika kipindi chote cha kuelekea uchaguzi Mkuu Octoba 31, mwaka huu. Hayo yamesemwa leo katika ufunguzi wa mkutano baina ya vyama vya siasa na NEC na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame,uliofanyika Paradise Hoteli Jijini Dar es Salaam na kuwataka viongozi hao kutambua wajibu wao wa kuelekea uchaguzi mkuu. Aidha alisema umefika wakati kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhamasisha wananchi kupitia mikutano ya kampeni umuhimu wa amani na kuhakikisha wanaweka mawakala katika vituo vya uchaguzi ili kuepuka malalamiko. "Sasa umefika wakati kwa vyama vya siasa kutambua wajibu wao ni vema mkahubiri amani na utulivu na kuhakikisha mnaweka mawakala mnaowaamini katika vituo vya kupigia kura, tunajua tunachangamoto ya kupokea malalamiko toka kwa vyama vya siasa kuhusu mwenendo wa uchaguzi na tunayashughulikia kwa wakati" alisema Jaji Makame. Hata hivyo Jaji Makame, alisema hivi sasa NEC, imeshafanya maandalizi ya kutosha na kusambaza vifaa vya uchaguzi katika majimbop yote nchini.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Lewis Makame, Mjumbe wa tume Omar Makungu Makamu Mwenyekiti, Prof. Amon Chalila Mjumbe na Mary Longway Mjumbe.
No comments:
Post a Comment