header

nmb

nmb

Thursday, September 2, 2010

MISHAHARA YA WALIMU WAKUU MANYONI YASIM AMISHWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA!!

Na Hillary Shoo,

Manyoni.

HALMASHAURI ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida imesimamisha mishahara ya walimu wakuu wa shule za sekondari 35 za wilaya hiyo kutokana utoro kazini.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo,Fourtunata Mallya aliyasema juzi wakati alipokuwa akifunga semina ya walimu wakuu wa shule za sekondari za wilayani humo.

Malya alisema mwalimu anapoajiriwa na Halmashauri ya wilaya hana budi kutii masharti yote yaliyowekwa katika kutekeleza majukumu yao .

“ Kama mlikuwa hamfahamu ni kwamba mtumishi anapoajiriwa na Halmashauri hatakiwi kusogea kwenda popote,si uhamisho si kwenda kusoma mpaka baada ya miaka mitatu huo ndiyo mkataba.”alisisitiza Malya.

“Na akienda kusoma akirudi hataweza kwenda tena mpaka muda huo huo uishe,mtumishi akiajiriwa haturuhusu uhamisho mpaka baada ya miaka mitatu,mwingine akiajiriwa, wanafanya ni sehemu ya kuchukulia check namba.”

“Mna fursa ya kwenda kusoma lakini fursa kwa utaratibu ebu tujaribu kuangalia nina walimu wangapi,waende basi kwa zamu kama wapo watano aende mmoja akirudi anaenda tena mwingine.”Alisema Mallya.

Akisoma risala kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo,katibu wa semina hiyo, Didasi Isuja aliiomba serikali wilayani humo kuangalia uwezekano wa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye shule zilizoko wilayani hapa.

Hata hivyo walimu hao hawakusita kutoa mapendekezo yao kuwa yana lengo la kuboresha sekta hiyo ya elimu ya sekondari.

Mafunzo haya yaliyohudhuriwa na wakuu wa shule 29 yaliandaliwa na idara ya elimu ya shule ya sekondari wilaya ya Manyoni.

No comments:

Post a Comment