header

nmb

nmb

Tuesday, September 14, 2010

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (kushoto) akisisitiza jambo kuhusu sanaa ya unenguaji nchini.Katikati ni mwasilishaji wa mada,Mama Nsao Shalua na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.
Sehemu ya umati wa wadau wa Sanaa ukifuatilia kwa makini kauli kuhusu unenguaji zilizokuwa zikitolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego (hayuko pichani).

Na Alistide Kwizela,BASATA. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa Bendi kuacha mara moja tabia ya kuwadhalilisha wacheza shoo (wanenguaji) kwa kuwavalisha mavazi ya kutia aibu na yanayodhalilisha utu wao.

Aidha,BASATA imewataka wanenguaji hao kuthamini utu wao na kufikiria upya dhana kwamba bila kuvaa nusu uchi basi sanaa ya muziki wa dansi haiwezi kupata soko na kuvutia watazamaji wengi kwenye maonyesho.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa kwa pamoja na BASATA na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) na kufanyika kila Jumatatu,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, lazima wadau wa muziki wa dansi wafikirie upya na kubadili mara moja tabia ya kuendekeza maonyesho yanayochafua maadili ya mtanzania.

ZAIDI TEMBELEA BLOG YA MICHUZI TAFADHARI

No comments:

Post a Comment